Machakos: Polisi wakamatwa kwa kuibia wanafunzi wa chuo kikuu simu

Polisi hao walitumia nguvu kuwaibia wanafunzi hao simu na vitu vingine vya thamana.

Muhtasari

• Wanafunzi hao walikuwa wakielekea chumba chao cha kukodi waliposimamishwa na askari hao.

• Afisa mmoja alimshika mwanafunzi mmoja na kuanza kumpiga makofi huku akimwimbia simu yake.

Afisa wa polisi akamatwa akimwimba mwanafunzi wa chuo kikuu
DCI Afisa wa polisi akamatwa akimwimba mwanafunzi wa chuo kikuu
Image: Radio Jambo

Afisa mmoja wa polisi alikamatwa kwa makosa ya wizi baada ya kumvamia mwanafunzi wa chuo kikuu cha Machakos na kumpokonya simu yake na vitu vingine vya thamana.

Afisa huyo, Kevin Sila  na mwandani wake David Muringu walikuwa wamewaandama wanafunzi  hao wawili walipokuwa wakiendesha baiskeli kuelekea kwenye chumba chao cha kukodi usiku wa Jumapili.

Afisa hao wa polisi waliokuwa na pikipiki yenye nambari ya usajili KMTE 363W waliwasimamisha wanafunzi hao mwendo wa asubuhi na kuanza kumchapa mmoja wao kwa makofi kwa kishindo huku wakimwibia mfuko wake.

Wanafunzi baada ya kupokea kichapo hicho walipata nafasi ya kutoroka huku wakipiga kamsa na kuwavutia majirani ambao walikuwa wanafunzi wenzao kutoka chuo hicho.

Wanafunzi waliokuwa karibu walimiminika eneo la tukio bila kukawia na kumwokoa mwenzao kutoka kwa ghadhabu ya afisa huyo wa usamala.

Licha ya Afisa huyo kurejesha simu aliyokuwa ameiba, raia waliokuwa wapepandwa na mori walizua kizaazaa.

Afisa huyo aliokolewa na polisi kutoka kituo cha Machakos waliomkamata pamoja na mwenzake.

Polisi hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya wizi kwa kutumia vurugu.