Chifu mkuu mstaafu ashtakiwa kwa kumnajisi msichana wa shule

Inadaiwa alitenda kosa hilo katika eneo la Kaptagat Kerio Valley ndani ya Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Muhtasari
  • Sang ambaye pia ni afisa mstaafu wa GSU na ana umri wa miaka 68 aliachiliwa kwa bondi ya sh 200,000 na udhamini sawa na huo
CHIFU MSTAAFU WILLIAM SANG
Image: MATHEWS NDANYI

Chifu mkuu mstaafu katika mji wa Eldoret William Sang ameshtakiwa kwa kumnajisi msichana wa shule siku ya Boxing day Desemba mwaka jana.

Chifu huyo alifika mbele ya hakimu mkazi mkuu Christine Menya na kukana mashtaka mawili ya unajisi.

Inadaiwa alitenda kosa hilo katika eneo la Kaptagat Kerio Valley ndani ya Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Sang ambaye pia ni afisa mstaafu wa GSU na ana umri wa miaka 68 aliachiliwa kwa bondi ya sh 200,000 na udhamini sawa na huo.

Menya aliamuru kesi hiyo itajwe Februari 6 kwa mkutano wa awali wa kesi hiyo.

Wakati huo huo hakimu alieleza kushangazwa na ongezeko la kesi ambapo vijana wengi wamefunguliwa mashtaka ya kutishia kuwaua mama zao mkoani humo.

Aliuliza upande wa mashtaka kujua kwa nini kumekuwa na ongezeko la kesi kama hizo.

Alitoa maoni hayo baada ya zaidi ya vijana 10 kushtakiwa tofauti kwa makosa ya kutishia kuwaua mama zao.