Washukiwa waliokamatwa kwa madai ya kuuza mechi waachiliwa kwa dhamana

Waliahidi kumlipa Otieno 14000 USD mwishoni mwa mechi kitendo ambacho kingeweza kuathiri matokeo ya mchezo.

Muhtasari
  • Wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Februari 3 na Machi 10 huko Roysambu ndani ya Kaunti ya Nairobi.
Akhiad kubev,(raia wa Urusi), Benard Nabende(raia wa Uganda) na Martin Munga(raia wa Kenya) walishtakiwa kwa kula njama ya kudanganya katika mchezo wa soka
Image: CAROLYNE KUBWA

Mkenya mmoja na raia wawili wa kigeni waliokamatwa kwa madai ya kutoa hongo na kuuza mechi  walishtakiwa Jumatatu mbele ya mahakama ya Makadara.

Akhiad kubev,(raia wa Urusi), Benard Nabende(raia wa Uganda) na Martin Munga(raia wa Kenya) walishtakiwa kwa kula njama ya kudanganya katika mchezo wa soka wa kupanga matokeo.

Wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Februari 3 na Machi 10 huko Roysambu ndani ya Kaunti ya Nairobi.

Watatu hao walikabiliwa na shtaka lingine kwamba mnamo Machi 10 huko Roysambu katika Kaunti ya Nairobi, na wengine hawakufikishwa mahakamani, kwa kutumia mbinu ya ulaghai walimshawishi Samson Otieno ambaye ni meneja wa timu ya city ​​stars kutoa upangaji wa mechi za city stars dhidi ya sofa paka FC.

Mchezo huo ulisemekana ungechezwa katika uwanja wa Ruaraka, Kenya Breweries mnamo Machi 11 saa 1500.

Waliahidi kumlipa Otieno 14000 USD mwishoni mwa mechi kitendo ambacho kingeweza kuathiri matokeo ya mchezo.

Walikanusha mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Eric Mûtûnga wa Mahakama ya Sheria ya Makadara na kuomba masharti nafuu ya bondi.

Waliachiliwa kwa bondi ya Sh300,000 na wadhamini wawili wa kiasi sawa.