Itumbi aachiliwa katika kesi ya kudai kulikuwa na njama ya kumuua Rais Ruto

Katika kuwaachilia Itumbi na Gateri, mahakama ilitaja mchakato mzima wa kuwashtaki wawili hao kuwa ukiukaji wa katiba.

Muhtasari
  • Huku Itumbi akizungumzia suala hilo, aliwasuta walio kuwa mawaziri  wa usalama wa Serikali ya Uhuru.
DENNIS ITUMBI
Image: KWA HISANI

Dennis Itumbi sasa yuko huru baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji kuondoa kesi kwa kukosa ushahidi dhidi ya madai yaliyotolewa kwamba kulikuwa na njama ya kumuua Rais William Ruto mwaka 2021 alipokuwa Naibu Rais.

Katika kuwaachilia Itumbi na Gateri, mahakama ilitaja mchakato mzima wa kuwashtaki wawili hao kuwa ukiukaji wa katiba.

Katika kesi hiyo, Itumbi alikabiliwa na makosa matatu likiwemo la kutengeneza hati ya uongo, kuchapisha taarifa ya uongo na kupanga upya simu yake ya mkononi. Alikanusha mashtaka yote.

Barua ambayo Itumbi alishtakiwa kwa kughushi ilidai kuwa kundi la maafisa wa ngazi za juu serikalini katika serikali ya aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta walifanya mkutano katika Hoteli ya La Mada, nje ya Barabara ya Thika jijini Nairobi kupanga madai ya mauaji ya Ruto.

Itumbi baadaye alikamatwa na kushtakiwa kwa barua hiyo ambayo iligundulika kuwa ilishirikiwa katika Kundi la WhatsApp lililopewa jina la vuguvugu la Tanga Tanga.

Huku Itumbi akizungumzia suala hilo, aliwasuta walio kuwa mawaziri  wa usalama wa Serikali ya Uhuru.