HAKI KWA FAMILIA YA MWATHI

Uchunguzi maalum wa kifo cha Jeff Mwathi kuanza Agosti 10

Yeyote mwenye ushahidi kuhusu kifo cha Mwathi ajitokeze ndipo familia yake ipate haki.

Muhtasari

•Mwathi, anadaiwa kufariki baada ya kujirusha kutoka jumba la ghorofa 12 mtaani Kasarani.

•Iwapo kuna mtu anaweza kuwa na ushahidi kuhusu kifo cha mwanetu, anaweza kuja kunieleza au  akaueleze katika idara yoyote inayoshughulikia maswala ya uchunguzi na upelelezi. Hili litatufaa sana kubaini kifo chake na haki itafanyika.

DJ Faxto anayeshukiwa kwa kifo cha Mwathi
DJ Faxto anayeshukiwa kwa kifo cha Mwathi
Image: HISANI

Mahakama ya Milimani jijini Nairobi imeahidi kuanzisha uchunguzi wa kina kufuatia kesi inayohusu kifo cha mbunifu wa mapambo Jeff Mwathi kilichotokea katika makao ya mwanamuziki DJ Faxto.

Mwathi, anadaiwa kufariki baada ya kujirusha kutoka jumba la ghorofa 12 mtaani Kasarani. 

Wakili wa familia ya Jeff Mwathi, Danstan Omari, anaamini kuwa haki itapatikana wakati uchunguzi huo utakapoanza Agosti 10.

Wakili huyo pia aliendelea kueleza kuwa, iwapo kuna mtu yeyote mwenye ushahidi wowote kuhusu  kifo cha Jeff Mwathi, amweleze mamake Mwathi au afisa yeyote wa polisi.

“We are appealing as a family, that anybody who has information, anybody, who has information to the circumstances that led to the death of the young man Jeff Mwathi can directly contact the family, can directly contact his lawyers, am here, so that we are able to produce that evidence necessary for justice.“  (Wakili huyo alisema ambayo yanatafsiriwa; Tafadhali kama familia, tunamsihi mtu yeyote, yeyote anaweza kuwa na ujumbe wowote kuhusu kifo cha kijana Jeff Mwathi anaweza kuwasiliana na familia yake moja kwa moja, au kuwasiliana na na mawakili wake, niko hapa.Ili tuuwasilishe ushuhuda wa kutosha kupatikana haki).

Omari pia alielezea machungu yanayomkabili mamake Jeff Mwathi, kwani alikuwa  tu na watoto wawili na kwa sasa amesalia na mmoja, huku akitaka haki itekelezwe .

“This mother had only two living children, one has gone, she is remaining with every one. Its very emotional. (We request that may justice prevail. (Huyu mama, alikuwa na watoto wawili waliokuwa hai, sasa mmoja ameenda. Inasikitisha sana na tunaomba kuwa haki itafanyika). Omari alisema.

Kwa upande wa Anne Mwathi mamake marehemu, hakuwa na jingine ila kuwashukuru Wakenya ambao wamekuwa pamoja naye tangu alipopatwa na msiba huo, huku akiamini kuna nafasi ya haki kufanyika.

“Mimi naitwa Anne Mwathi, na kile ambacho ningesema kwanza ni kuwashukuru Wakenya wote humu nchini na hata wale wako Amerika na middle east kwa kusimama nami tangu nilipopatwa na haya; naamini kuna nafasi ya haki kufanyika.” Mama Mwathi alisema.

Haya yanajiri wakati ambapo mashahidi 35 tayari wamejitokeza na kuwa tayari kutoa ushahidi wakati uchunguzi huo utakapoanza.