Mahakama moja katika kaunti ya Kisii imemhukumu mwanamume mmoja kifungo cha hadi miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka ajuza wa miaka 80.
James Mireri Akunga anasemekana kumvizia ajuza huyo katika nyumba yake mwaka 2010 mwendo wa saa nne usiku ambapo alimkanyagia chini na kumtendea unyama huo, Gazeti la The Star limeripoti.
Siku iliyofuatamkaza mkaza mwana alipomtembelea katika nyumba yake mwendo wa saa nne asubuhi, alimpata ajuza huyo amelala hoi bin taabani.
Alikuwa amelala kwa maumivu makali kitandani na kwenye blanketi lake kulikuwa na matoke ya manii ya mwanamume pamoja kinyesi na damu.
Hapo ndipo alimueleza mkaza mwana wake kwamba alibakwa na pia waliweza kumtambua kijana huyo.
Ajuza huyo alikimbizwa katika hospitali ya Keumbu ambapo alifanyiwa vipimo vya afya na kupewa matibabu.
“Mwathiriwa alikuwa na chembechembe za damu katika sehemu zake nyeti na alikuwa katika maumivu makali. Pia chembechembe za manii zilipatikana na ilibainika kwamba alikuwa amebakwa,” nyaraka za mahakamani zilisema.
Akunga alitiwa mbaroni Machi mwaka 2011 na alipatikana mafichoni baada ya kutoroka nyumbani na alidakwa baada ya kurejea nyumbani kwa ajili ya mazishi ya dadake.
Mahakamani alipigwa miaka 30 jela lakini alikata rufaa katika mahakama ya juu.
Pia kesi hiyo yake ilikwenda hadi katika mahakama ya rufaa ambapo alipinga vikali jinsi alivyohukumiwa. Alilalamika kwamba wakati bibi huyo alibakwa kulikuwa na giza na huenda alimfananisha na mtuhumiwa aliyemtendea unyama huo.
Zaidi ya kumtambua mshukiwa, ajuza huyo alikiri mahakamani kwamba alikuwa na tatizo la kuona na hakuweza kumuona vizuri mshukiwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi iliyoendeshwa mchana peupe. Katika hili, mshukiwa anahisi kwamba hakukuwa na ushahidi kwamba ukosefu wa macho ungepelekea yeye kudhulumiwa.
Mwisho wa siku, jopo la majaji watatu katika hukumu iliyotolewa Julai 21 walibaini kwamba chumba hicho kilikuwa na mwanga na pamoja na kwamab kijana huyo alikuwa jirani, angeweza kutambuliwa bayana.
Majaji hao walisema kwamba kifungo chake cha miaka 30 alichokabidhiwa kinastahiki.