• Uchunguzi wa baada ya maiti uligundua alikuwa amepata "majeraha mengi na makubwa".
Baba, mama wa kambo na mjomba wa Sara Sharif wameshtakiwa kwa mauaji ya msichana wa miaka 10, Polisi wa Surrey wamesema.Urfan Sharif, 41, mpenzi wake Beinash Batool, 29, na kakake Urfan, Faisal Malik, 28, wote kutoka Hammond Road, Woking, wamefunguliwa mashtaka.
Pia kila mmoja ameshtakiwa kwa kusababisha au kuruhusu kifo cha mtoto.
Mwili wa Sara ulipatikana nyumbani kwao tarehe 10 Agosti.Uchunguzi wa baada ya maiti uligundua alikuwa amepata "majeraha mengi na makubwa".
Watu wazima watatu waliondoka Uingereza kwenda Pakistan tarehe 9 Agosti.Walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Gatwick Jumatano jioni baada ya kushuka kutoka Dubai.
Mapema Ijumaa asubuhi, Polisi wa Surrey walithibitisha kuwa wamefunguliwa mashtaka.Wamerejeshwa rumande ili kufika katika Mahakama ya Guildford baadaye siku ya Ijumaa.