Mahakama ya Makadara imeombwa na mawakili wa aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga, kuagiza polisi kumpa ulinzi dhidi ya maafisa wa polisi kutokana na kudhulumiwa kwa uhuru wake.
Mawakili wanaomwakilisha Njenga walimweleza hakimu mkuu wa Makadara, Tito Gesora, Jumatatu kwamba Jumamosi jioni mwendo wa saa 10 jioni, Njenga alitekwa nyara na polisi waliokuwa wamejifunika nyuso zao .
wakili Ndegwa Njiru aliambia mahakama kuwa aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga ameshtakiwa kwa kumiliki rungu na silaha nyingine.
Hata hivyo, ameachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Sh100,000. Kiongozi huyo wa zamani w Sasa anadai kuwa anajua polisi ndio walimteka nyara.
Mahakama ilisikiza zaidi Njenga alitupwa katika eneo la Limuru Banana Estate baada ya watu waliomteka nyara kumuacha huru.
Wakili Evans Ondieki aliuliza mahakama ni kwa nini afisa wa serikali anapaswa kujifunika kichwa wakati ambapo anamkamata mtu.
"Anapaswa kutoa heshima kwa ofisi, ni wahalifu pekee wanaoficha sura zao." Ondieki aliongeza kuwa utekaji nyara huo huenda ukaingilia na kuathiri matokeo ya kesi iwapo Njenga hangeachiliwa.
Njenga alikuwa kortini kwa ajili ya kusikizwa kwa kesi yake ambapo alishtakiwa kwa kumiliki panga na rungu miongoni mwa silaha nyingine hatari.
Mawakili hao pia waliomba vitu vilivyochukuliwa zikiwemo simu za mikononi na polisi virejeshwe kwa washtakiwa.
Upande wa mashtaka hata hivyo ulisema walihitaji kutajwa zaidi kwa afisa wa upelelezi ili kufafanua juu ya vielelezo hivyo.