Google maps yashtakiwa kwa kumuelekeza mtu kuendesha gari kwa daraja lililovunjika

Dereva huyo alikuwa akifuata maelekezo ya Google Maps usiku akitoka katika tafrija ya kusherehekea birthday ya bintiye wakati aliendesha gari kwenye daraja hilo lililoporomoka na kuanguka futi 20 hadi kufa.

Muhtasari

• Paxson aliendesha gari nje ya ukingo usio na kizuizi wa daraja huko Hickory, North Carolina, na kuzama, nyaraka za kesi zilinukuliwa na runinga hiyo.

• Kesi hiyo ilidai kwamba Google walipokea malalamishi kutoka kwa watu wakiwataka kurekebisha ramani yao lakini hawakusikia.

Google Maps
Google Maps
Image: Google

Kampuni ya kutoa huduma za kijiditali za ramani, Google Maps imejipata pabaya baada ya kudaiwa kumuelekeza mtu mmoja kuendesha gari kwa daraja ambalo lililovunjika kupelekea kifo chake.

Kwa mujibu wa runinga ya CNN, familia ya mtu huyo aliyefariki sasa imeichukulia hatua za kisheria Google Maps ikidai kwamba mwelekezo wa ramani ambayo walitoa kwa mpendwa wao kwenye daraja hilo lililovunjika ndio yalisababisha kifo chake baada ya gari lake kutumbukia takriban futi 20, kulingana na kesi hiyo.

Philip Paxson alikuwa akifuata maelekezo ya Ramani za Google alipokuwa akiendesha gari nyumbani usiku wa manane mnamo Septemba 2022 kutoka kwa sherehe ya miaka 9 ya kuzaliwa kwa binti yake wakati mfumo wa Google Maps ulipomwelekeza kupita kwenye daraja lisilo na alama na lisilo na kizuizi ambalo lilikuwa limeporomoka miaka iliyopita, CNN waliripoti.

Paxson aliendesha gari nje ya ukingo usio na kizuizi wa daraja huko Hickory, North Carolina, na kuzama, nyaraka za kesi zilinukuliwa na runinga hiyo.

Wakili wa familia ya Paxson Robert Zimmerman alisema katika taarifa:

 "Tumegundua kuwa Ramani za Google ziliwaelekeza vibaya madereva kama Bw. Paxson kwenye barabara hii iliyoporomoka kwa miaka mingi, licha ya kupokea malalamiko kutoka kwa umma kutaka Google kurekebisha ramani na maelekezo yake ili kuashiria kuwa IMEFUNGWA."

Kesi hiyo inadai majirani walikuwa wameelezea wasiwasi wao kuhusu Ramani za Google kuwaongoza madereva juu ya daraja hilo, ambalo inadaiwa halijakarabatiwa tangu lilipoporomoka sehemu yake mwaka wa 2013.