Brian Mwenda aachiliwa kwa dhamana ya Ksh.200K

Njagi alikamatwa na maafisa wa upelelezi wa DCI mnamo Oktoba 18 baada ya kufichuliwa kuwa wakili bandia.

Muhtasari
  • Katika kutoa dhamana, Hakimu Mkuu wa Milimani, Lukas Onyina, alisema upande wa mashtaka haukutoa sababu za msingi za kuwanyima dhamana mshtakiwa.
Wakili bandia Brian Mwenda.
Wakili bandia Brian Mwenda.
Image: Hisani

Mahakama ya Nairobi imemwachilia anayedaiwa kuwa wakili feki Brian Mwenda kwa dhamana ya Ksh.200,000 pesa taslimu.

Katika kutoa dhamana, Hakimu Mkuu wa Milimani, Lukas Onyina, alisema upande wa mashtaka haukutoa sababu za msingi za kuwanyima dhamana mshtakiwa.

Mwenda wiki iliyopita alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka sita ya kutoa hati ya uongo, kutengeneza hati ya uongo pamoja na cheti cha kufanya kazi.

Alikanusha mashtaka yote mbele ya Hakimu Mkuu wa Nairobi Lukas Onyina.

Njagi alikamatwa na maafisa wa upelelezi wa DCI mnamo Oktoba 18 baada ya kufichuliwa kuwa wakili bandia.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 7.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama kumnyima Mwenda dhamana kwa madai kuwa iwapo ataachiliwa hatahudhuria kesi mahakamani.

Mahakama pia iliambiwa kwamba mwenendo wa Mwenda unaonyesha kwamba hajali sheria, na kwamba alikwepa polisi kwa zaidi ya siku nne.