Anne Adhiambo Ouma almaarufu Nut, mwanamke anayedaiwa kumuua afisa wa fedha wa Hospitali ya Nairobi Eric Maigo amekiri na kukubali kosa la mauaji.
Ouma, ambaye alitambuliwa kuwa amefikisha umri wa miaka zaidi ya 18 alifika mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanyi Kimondo na kukiri kutenda kosa hilo.
Hii ni baada ya karani wa mahakama kumsomea mara tatu kosa analodaiwa kutenda kwa lugha ya kiswahili, Hakimu hata hivyo, aliwaonya mshtakiwa dhidi ya matokeo ya kukiri hatia.
Ouma anawakilishwa na wakili Samuel Ayora, Kesi hiyo itatajwa Novemba 8 kwa ajili ya kusikilizwa katika Mahakama ya Kibera. Ouma yuko rumande katika Gereza la Wanawake la Lang'ata.
Alishtakiwa baada ya upande wa mashtaka kusema kwamba alikuwa anafaa kushtakiwa na tathmini ya umri ilionyesha kuwa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 18.
Mawakili wa upande wa utetezi, hata hivyo, walibishana kuhusu umri wake wakisema bado ni mtoto wa miaka 17. Upande wa mashtaka ulishikilia kuwa Ouma ni mtu mzima aliyefanyiwa uchunguzi na daktari aliyehitimu.
Jaji Kimondo aliagiza suala hilo kushughulikiwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Kibera Diana Kavedza. Katika shtaka lililosomwa kortini, Ouma anashtakiwa kuwa mnamo Septemba 15, katika mtaa wa Woodley, alimuua Eric Maigo Siku ya Jumatano.
Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Milimani Gilbert Shikwe alifunga maombi hayo mengine ambayo polisi walikuwa wametafuta muda zaidi wa kumzuilia akisubiri uchunguzi.
uchunguzi wao na ushahidi ulionyesha kuwa anahusishwa na kifo cha Maigo. Maigo aligunduliwa na majeraha ya kuchomwa kisu katika makazi yake ya Woodley Estate mnamo Septemba.