Ombi la kutaka Koome kung’atuliwa lawasilishwa kwa JSC

Kojo anahoji kuwa Koome hakuwa muwazi na kuwa aliwabagua watu ambao walikuwa wametuma maombi ya kuwa wanachama wa bodi.

Muhtasari

• Mlalamishi, Michael Kojo Otieno, anadai kuwa Jaji Mkuu alikosa kufuata sheria katika kuwateua wanachama wa mahakama ya rufaa ya ushuru. 

Jaji Mkuu Martha Koome
Image: BBC

Ombi limewasilishwa mbele ya Tume ya Huduma za Mahakama (JSC) kutaka Jaji Mkuu Martha Koome aondolewe afisini. 

Mlalamishi, Michael Kojo Otieno, anadai kuwa Jaji Mkuu alikosa kufuata sheria katika kuwateua wanachama wa mahakama ya rufaa ya ushuru. 

Kojo anahoji kuwa Koome hakuwa muwazi na kuwa aliwabagua watu ambao walikuwa wametuma maombi ya kuwa wanachama wa bodi. 

"Hatua za jaji mkuu katika kuteua wanachama zaidi ya mahitaji yaliyowekwa zilikiuka kifungu cha 4b cha Sheria ya Mahakama ya Rufaa ya Ushuru," Kojo anasema. 

Anasema kuwa kwa sababu za kukiuka sheria, jaji mkuu hafai kushikilia wadhifa huo na anapaswa kuondolewa madarakani.