Mahakama yabatilisha uteuzi wa Anthony Mwaura kama mwenyekiti wa KRA

Katika notisi ya gazeti la serikali ya Novemba 17, Ruto alisema Mwaura atahudumu kwa muda wa miaka mitatu.

Muhtasari
  • Jaji Francis Gikonyo alisema uteuzi wa Mwaura haukuwa halali jinsi ulivyofanywa alipokuwa akikabiliwa na mashtaka ya ufisadi.
Anthony Mwaura

Mahakama kuu imefutilia mbali uteuzi wa Anthony Mwaura kama Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA)

Jaji Francis Gikonyo alisema uteuzi wa Mwaura haukuwa halali jinsi ulivyofanywa alipokuwa akikabiliwa na mashtaka ya ufisadi.

Mwaura alikula kiapo Novemba 2022 baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

Katika notisi ya gazeti la serikali ya Novemba 17, Ruto alisema Mwaura atahudumu kwa muda wa miaka mitatu.

“Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 6(2) (a) cha Sheria ya Mamlaka ya Mapato ya Kenya, mimi, William Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi namteua Anthony Ng’ang’a Mwaura. kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mapato ya Kenya, kwa muda wa miaka mitatu (3), kuanzia tarehe 18 Novemba 2022," notisi ya gazeti la serikali ilisoma.