• Kwa upande wake, mwanamume huyo alisisitiza kwamba alifanya harusi ya kitamaduni kwa mujibu wa mila na desturi ya jamii ya waluo.
• Lakini alikosa kuonyesha ushaidi wowote kwamba alimuoa mwanamke huyo hivyo mahakama ikasema hakuna ndoa ya kuvunjwa pale kwani hawakuwa wameoana.
Mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo amepatwa na pigo la kudumu baada ya maakama kumtaarifu kwamba mke aliyeishi naye kwa miaka 22 si mkewe halali.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwenye gazeti la The Standard, mwanamume uyo alielekea mahakamani akitaka kuvunja ndoa yake iliyodumu kwa miaka 22 lakini baadae mahakama ikabaini kwamba hakuwahi kumuoa mkewe rasmi, hivyo katika miaka yote hiyo walikuwa wanaishi tu kama marafiki na wala si mke na mume.
“Wapenzi hao waliishi pamoja hadi Desemba 2020, mwanamke huyo alipohamia Marekani. Akiwa amehuzunishwa na kukataa kwake kurudi Kenya, mwanamume huyo, aliyepewa jina la JTO, alihamia mahakama ya hakimu kutaka kukatisha ndoa na mwanamke aliyejulikana kwa jina la AP,” The Standard waliripoti.
Katika kesi hiyo iliyoanzia kwenye mahakama ya chini kabla ya mwanamume huyo kukata rufaa kwenye mahakama ya juu, alikuwa anasisitiza kwamba alimuoa mwanamke huyo katika hafla ya kitamaduni bila stakabadhi zozote.
Jaji katika uamuzi wake, alisema kwamba hata kama walifunga harusi katika hafla ya kitamaduni, wangehitajika kuiandikisha ndoa yao rasmi kwenye taasisi husika ya serikali, lakini jamaa huyo hakufanya hivyo, na hivyo hakuwa na cheti chochote kuonyesha kuwa mwanamke huyo alikuwa mkewe.
Japo jamaa huyo alisisitza kwamba alimuoa kwa taratibu zote za mila ya jamii ya Wajaluo, hakuweza kuonyesha ushahidi wowote wa kufanyika kwa ndoa hiyo.
Mahakama iliamuru kwamba hakuna ndoa ya kuvunjwa pale kwani mwanzo wawili hao hawakuwa wameoana kwa sababu hakukuwa na ushahidi wowote wa kuthibitisha hilo.
"Kwa hakika, baada ya kupuuza kipengele cha usajili wa ndoa yake ya kimila, mrufani alifungiwa nje ya kutaka kuvunjika kwa aina yoyote ya muungano aliyoshiriki na mlalamikiwa," jaji alisema.