Raia wa kigeni wafungwa jela mwaka 1 baada ya kwa hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya

Raia wa kigeni wamepatwa na makosa ya ulanguzi wa dawa za kulevywa na mahakama ya JKIA

Muhtasari

• Korti yaamuru mihadarati iliyopatikana kuharibiwa na washukiwa kurudishwa nchini kwao baada ya kukamilisha kifungu ama kulipa faini

• Wawili hao walikamatwa na heroini na bangi katika eneo la Nyamakima, jijini Nairobi

Image: HISANI

Raia wawili wa kigeni kwa jina Kanu Arinze na Ebuka Titus wamehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au faini ya shilingi milioni moja.

Wawili hao wamepatikana na hatia ya ulanguzi wa dawa za kulevya na mahakama ya JKIA.

Mahakama hiyo imeamuru wawili hao kurejeshwa nchini kwao baada ya kumaliza kifungo chao ama baada ya kulipa faini.

Kanu na Titus walikamatwa Machi 13 2024 katika eneo la Nyamakima na maafisa wa polisi wa kitengo cha kupambana na dawa za kulevyakwa ushirikiano na maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha kukabiliana na uhalifu uliopangwa wa kimataifa.

Wawili hao nbaada ya kukamatwa na kufikishwa kizimbani, walikiri mashtaka dhidi yao na hatimaye mahakama hiyo kuwapata na hatia.

Ushahidi wa polisi dhidi ya raia hao wa kigeni ulionyesha kuwa baada ya raia hao kukamatwa waliwalelekeza maafisa wa polisi hadi sehemu yao ya maficho katika mitaa wa Umoja na Sunton ambapo polisi walinasa mihadarati,

 Dawa za kulevya aina ya heroini gramu 39.04 na bangi gramu 25.71 ilikamatwa maeneo hayo.

Korti iliamuru kuharibiwa kwa mihadarati iliyokamatwa na mbayo iliyokuwa sehemu ya ushahidi