Mahakama
ya Kabarnet katika kaunti ya Baringo imewafunga washukiwa wanne wa ubakaji miaka
15 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya ubakaji wa genge.
Kesi
hiyo iliyosikilizwa mbele ya hakimu Edwin Mulochi ilisema kuwa ushahidi
uliowasilishwa na mashahidi ulikuwa wa kutosha na wenye uzito mkubwa dhidi ya
washukiwa.
Hakimu
Edwin Mulochi aliwapata washukiwa hao kwa majina Benard Kiprop, Jackson Cheruiyot,
Kurgat Chebotibin na Benson Cheruiyot na hatia kinyume na kifungu cha 10 cha
sheria ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mashahidi
waliowasilishwa na Rebecca Bartilol walitoa ushahidi ambao mahakama ilitaja
kuwa ulionyesha hatia kwa washtakiwa bila shaka yoyote na kupita viwangovya
kisheria vinavyohitajika kwa ajili ya kutiwa hatiani.
Wafungwa
hao walipatikana na hatia ya kutekeleza ubakaji huo mnamo Septemba tarehe 24
mwaka wa 2023mwendo wa saa moja jioni katika kijiji cha Sirwet, kaunti ndogo ya
Baringo Kusini.