Aliyekuwa mkuu wa mauzo katika huduma ya vijana kwa taifa NYS
Hendrick Nyongesa amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana
na hatia ya kughushi stakabadhi kinyume na sheria kifungu cha 347(a) cha katiba
kilichosomwa kwa pamoja na kifungu cha 349 cha makosa ya adhabu.
Kesi dhidi ya Nyongesa iliwasilishwa mahakamani na ofisi ya
mwendeshaji wa amshtaka ya umma ODPP baada ya kudaiwa kutekeleza mashtaka
aliyosomewa mnamo Desemba mosi mwaka wa 2014.
Mahakama ilielezwa kuwa Nyongesa pamoja na washukiwa wengine ambao hawakuwa mbele ya mahakama hiyo
wakati wa kuhukumiwa, walighushi stakabadhi kwa madhumuni ya udanganyifu.
Nyongesa alipatikana na hatia ya udanganyifu wa kughushi
stakabadhi kutoka kwa wizara ya kazi ya umma ya kusambaza bidhaa kwa huduma ya
vijana klwa taifa NYS.
Vile vile mshukiwa huyo pia amehukumiwa kufungo kingine cha
miaka mitano kwa uvunjaji wa uaminifu kama mfanyakazi wa serikali katika huduma
ya umma.
Akitoa hukumu hiyo, jaji Wandia Nyamu pia amemhukumu aliyekuwa
mkurugenzi wa fedha wa NYS Samuel Wachenje kifungo cha miaka 5 jela bila chaguo
la kulipa faini.