Mahakama ya Kisumu imeagiza kufanyiwa uchunguzi wa akili kwa mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa meneja katika kampuni ya Wells Fargo Willis Ayieko baada ya kufikishwa mahakamani hapo Alhamisi.
Mshukiwa huyo alishtakiwa kwa hatia ya mauaji kinyume na kifungu cha 203 cha katiba kilichosomwa kwa pamoja na kifungu cha 204 cha kanuni ya adhabu katika sura ya 63 ya katiba ya Kenya.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Catherine Mwaniki, Patrick Okango na Soita Evans kupitia kesi iliyowasilisha mahakamani humo, ilisema kuwa mshukiwa huyo pamoja na washukiwa wengine ambao hawakufikishwa mbele ya mahakama hiyo allihusika katika mauaji ya Willis Ayieko kati ya tarehe 18 na 23 Novemba katika eneo la Nyambonga mpakani mwa kaunti ndogo za Gem na Khwisero.
Mshukiwa huyo aidha hakukana wala kukubali mashtaka dhidi yake akiwa mbele ya naibu msajili wa mahakama kuu Getrude Serem.
Naibu msajili wa mahakama kuu Serem, aidha aliamuru kufanyiwa kwa uchunguzi wa akili mshukiwa huyo kubaini ikiwa anaweza kujitetea mahakamani au la.
Mshukiwa huyo atafikishwa tena mahakani humo mnamo Desemba 18 mbele ya hakimu Roselyne Aburili.
Mwili wa Willis Ayieko ulipatikana siku chavhe ukiwa na majeraha baada ya kuripotiwa kupotea na gari lake kupatikana karibu na kituo kimoja cha petrol katika kaunti ya Vihiga.
Mshukiwa
huo anazuiliwa katika gereza la Kisumu maarufu kama Kodiaga akisubiri kufanyiwa
vipimo vya akili kabla ya kurejeshwa mahakamani.