Idara ya upelelezi ya DCI imeonya umma dhidi ya genge la wahalifu ambalo limeibuka kwenye biashara ya shamba ambapo linaghushi stakabadhi za umiliki wa shamba kwa malengo ua kufaidika na hela zinazotolewa kwenye biashara hiyo. DCI imesema kwamba walaghai hao wanalenga vitongoji vilivyoimarika wakilenga wamiliki wa shamba ambao wanawekeza kwa ushirikiano na wawekezaji.
Kwa mujibu wa DCI, wahalifu hao wa kijasiriamali huibuka wakati wawekezaji hutafuta shamba ambazo watawekeza ndani yake ambapo wanajidai kutoa vyeti vya kukodisha kwa wamiliki rasmi wa shamba. Vyetihivyo kwa mujibu wa DCI, ndivyo vinatumiwa na wahalifu hao kutekeleza ulaghai.
Idara hiyo aidha imerejelea kisa ambapo mkaazi mmoja wa eneo la Pumwani nusra apoteze vipande vyake 2 vya ardhi isingelikuwa mwekezaji makini kutafuta huduma za mwanasheria aliyefanya uchunguzi kamili. Hata hivyo, mmiliki huyo wa shamba alipoteza shilingi 553,550 kwa mlaghai aliyejifanya kuwa mfanyakazi katika ofisi ya msajili wa mashamba katika kaunti ya Nairobi.
Hata hivyo mshukiwa mmoja amekamatwa kutokana na kisa cha
Pumwani na anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya Milimani mnamo Jumanne
kujibu mashtaka dhidi yake. Mshukiwa huo anadaiwa kuongoza genge la walaghai
ambao walitoa cheti bandia kwa mmiliki
mmoja wa shamba eneo la Pumwani.
Uchunguzi wa DCI umeonyesha kuwa walaghai hao ni
sehemu ya walanguzi wa dhahabu bandia ambao wameamua kutuliza biashara ya
dhahabu na kuingilia biashara ya shamba.