Mahakama ya Kabarnet katika kaunti ya Baringo mnamo Jumatano Disemba 4, ilimhukumu mwanamume mwenye umri wa makamu kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya unajisi.
Mahakama hiyo kupitia hakimu Purity Koskei, ilimpata mshukiwa na hatia hiyo baada ya upande wa uendeshaji mashtaka kuwasilisha ushahidi wa kutosha mbele ya mahakama.
Upande wa mashataka, katika kesi iliyowasilisha mbele ya mahakama hiyo, iliwasilisha ushahidi wa kutosha kutoka kwa mashahidi 6 kwenye kesi hiyo, ambao walifanikisha upande wa mashtaka kubaini vipengele vyote vinavyohitajika vya kosa lililotekelezwa na mshukiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umaa ODPP, ushahidi wa upande wa mashtaka ukiongozwa na Collins Ogutu, ulichora taswira kamili ya hatia ya mshukiwa mahakama ikibaini kwamba ushahidi huo ulikuwa zaidiya kutiliwa shaka.
Hata hivyo mshukiwa alipatikana na hatia kinyume na na
kufungu cha 3(1) cha katiba kilichosomwa kwa pamoja na kifungu cha 3(3) cha
sheria ya vitendo vya ngono namba 3 ya mwaka 2006.