logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mahakama yaamuru Airtel kumlipa Willis Raburu milioni 5 kwa kutumia nembo yake 'Bazu'

Mwanahabari huyo mashuhuri aliiambia mahakama kwamba alikuwa amesajili rasmi nembo ya biashara ya ‘Bazu.’

image
na

Mahakama11 March 2024 - 13:16

Muhtasari


•Mahakama ya Milimani imeamuru Airtel Kenya Limited kumlipa mwanahabari Willis Raburu KSh5 milioni pamoja na fidia ya ziada .

•Mwanahabari huyo mashuhuri aliiambia mahakama kwamba alikuwa amesajili rasmi nembo ya biashara ya ‘Bazu.’

Wilis Raburu

Mwanahabari Willis Raburu, mkurugenzi wa huduma za kidijitali na Ubunifu katika Cape Media amezamia kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii kusherehekea ushindi wake dhidi ya Airtel.

Willis Raburu aliishtaki Airtel Kenya kwa kutumia nembo yake ya biashara iliyosajiliwa bila kupata idhini inayohitajika.

Mahakama ya Biashara ya Milimani imeamuru Airtel Kenya Limited kumlipa mwanahabari Willis Raburu KSh5 milioni pamoja na fidia ya ziada kwa kutumia chapa yake ya biashara, ‘Bazu’.

Mwanahabari huyo mashuhuri aliiambia mahakama kwamba alikuwa amesajili rasmi nembo ya biashara ya ‘Bazu.’

Raburu alitoa shukrani zake kwa hukumu iliyotolewa hivi karibuni na Mhe. Rawlings Museiga katika mahakama ya Milimani, akiongeza kuwa inawajibisha Airtel Kenya kwa kukiuka nembo yake ya biashara iliyosajiliwa 'BAZU'.

Willis pia aliitambua Airtel Kenya kama chapa na biashara inayoheshimika lakini pia alisisitiza jinsi ilivyokuwa muhimu kwake kulinda chapa na jina lake chini ya chapa ya biashara ya 'BAZU'.

Mkurugenzi huyo wa huduma za kidijitali na ubunifu wa Cape media katika taarifa yake alisisitiza zaidi kwamba heshima ya haki miliki ni muhimu, na wale wanaotumia jina la BAZU bila mamlaka watakabiliwa na matokeo sawa na kuongeza kuwa notisi za kisheria tayari zimetolewa.

Raburu mnamo Juni 24, 2022 alishtaki kampuni ya mawasiliano kwa kutumia chapa yake ya biashara ‘Bazu’ katika kukuza mpango wake mpya wa ‘Bazu Bundle’.

Kupitia wakili wake Victor Orandi wa Mathew and Partners Advocates, Raburu aliwasilisha kesi hiyo katika Mahakama Kuu lakini Mei 9, 2023, ikahamishiwa kwa mahakama ya hakimu.

Mahakama pia iliipa Airtel Kenya muda wa siku 45 kabla ya kutekeleza amri na kampuni imsema inaweza kukata rufaa ndani ya muda uliotajwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved