Covid-19: Watu 523 wapatikana na corona 11 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 523 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 6,469 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 185,060 kutoka kwa sampuli 1,970,001
  • Katika visa hivi vipya, 503 ni raia wa Kenya huku 20 akiwa raia wa kigeni, 310 ni wa kiume na 213 ni wanawake

Kenya imerekodi visa 523 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 6,469 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 185,060 kutoka kwa sampuli 1,970,001.

Katika visa hivi vipya, 503 ni raia wa Kenya huku 20 akiwa raia wa kigeni, 310 ni wa kiume na 213 ni wanawake.

 

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana wiki 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 99.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 8.1%.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 86 wamepona virusi vya corona,50 walipona wakiwa nyumbani huku 36 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 126,680 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 11 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,651 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,136 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 5,856 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 127 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU