'Kufaulu kwa familia yangu ni kwa sababu ya mke wangu,'DP Ruto amlimbikizia mkewe sifa

Muhtasari
  • DP Ruto amlimbikizia mkewe sifa
  • Pia  ni matamanio ya kila wanandoa kuona familia na ndoa yao imedumu
  • Akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo Naibu rais William Ruto,alimlimbikizia mkewe sifa kwa kufaulu kwa familia yake
Mtangazaji Gidi na Naibu rais William Ruto
Image: Douglas Okiddy

Ni furaha ya kila wanandoa kuona familia na ndoa yao ikiendelea bila ya changamoto zozote au kukosana kati ya wapenzi hao wawili.

Pia  ni matamanio ya kila wanandoa kuona familia na ndoa yao imedumu.

Akiwa kwenye mahojiano na Radiojambo Naibu rais William Ruto,alimlimbikizia mkewe sifa kwa kufaulu kwa familia yake.

Kulingana na Ruto mkewe Rachel amekuwa akimuombea na kumsaidia katika kazi yake, zaidi ya yoe alisema kwamba amekuwa akimuelewa.

Wawili hao sasa wamekuwa katika ndoa kwa zaidi ya miaka 25.

"Kufaulu kwa familia yangu ni kwa sababu ya mke wangu maanake nilipata mke karibu na malaika na ni bahati tu ya Mungu

Kupata mke ambaye anakusaidia, anakuelewa, anakuombea, hapo ndio unapata bahati ya kupiga hatua kwenda mbele." Ruto Alisema.