Rufftone: Nimejiunga na UDA kwa sababu mawazo yetu ni sawa

Muhtasari
  •  Aidha amesema kwamba, atahakikisha rasmali za serikali zinawafikia wananchi na kutumika ipasavyo bila visa vyovyote vya ufisadi
  • Rufftone ametoa ombi kwa wakazi wa kaunti ya Nairobi kumpigia kura na pia kudumisha amani na pia kupiga teke dondandugu la ukabila ambalo limekumba taifa hili kwa muda

Mgombea wa kiti cha useneta katika kaunti ya Nairobi, Roy Smith Mwatia almaarufu Rufftone amesema kwamba ameungana na mrengo wa naibu rais William Ruto kwa kuwa azma na ndoto zao kwa wananchi zinaoana.

Akizungumza na Radio Jambo Alhamisi tarehe 27/01/2022, Mwatia amesema kwamba kwa muda mrefu sasa, vijana katika taifa hili wametumika kama vyombo vya kupiga kura pasi  na maisha yao kuboreshwa. Kulingana naye, chama cha UDA kina muundokazi ambao utasaidia kuboresha hali za vijana na wanachi wote kwa ujumla baada ya uchaguzi.

Amewarai viongozi kutambua mchango wa vijana katika uchumi wa taifa hili na hivyo basi kuwashirikisha katika mikakati ya kimaendeleo na kuwasaidia kuafikia ndoto zao na zile za familia zao.

Rufftone amesema kwamba kwamba anawania nafasi ambayo haina mgao wowote kutoka kwa serikali kuu, hiyo ikionyesha kwamba amejitolea kuleta suluhu kwa matatizo ambayo yamekuwa yakiwazonga wananchi.

"The reason why i'm vying for a senatorial seat is one,i believe it's a selfless legislative office, why, because it does not have a budget.If you come in a senator, it means truly you have the heart for the people," alisema Rufftone.

RUFFTONE
RUFFTONE
Image: HISANI

Msanii huyu ambaye pia ni balozi wa uhusiano mwema  katika taifa la Korea Kusini, amesema kwamba iwapo wananchi wa Nairobi watamchagua kuwa Seneta wao, atahakikisha anapea kipaumbele ukuaji wa viwanda ili kutoa nafasi za kazi kwa vijana ambao ni asilimia kubwa ya idadi ya watu hapa Kenya. Vilevile amesisitiza kwamba atatumia maarifa ambayo ameyapata katika mataifa ya kigeni kama vile Dubail na Korea Kusini kuhakikisha ndoto hii inafanikiwa.

Akizungumzia masuala ya ghasia za baada ya uchaguzi, amewaomba vijana kutojihusisha na vurugu hizo na badala yake kudumisha amani wakati na baada ya kipindi cha uchaguzi. Amesema kuwa kutofautiana katika mawazo hakufai kuwa sababu ya kuzua hali ya taharuki nchini.

" Sijawahi elewa kwa nini wakati vijanaa wanaona ball, wakikatiana jambo la ukabila halitokei  lakini ikifika time ya siasa wanaanza kugawana kwa misingi ya kikabila  na kadhalika, our differences are our beauty," msanii huyo alisema.

Radio Jambo Kenya | Ongea Usikike | Ni kituo nambari moja Kenya kwa matangazo ya kiswahili. Vipindi vyake vina jumuisha Spoti,Mijadala moto moto na muziki wa Kiafrika #RadioJamboKenya Subscribe to RadioJambo Youtube - https://bit.ly/39wwc6u Mitandao ya Kijamii Instagram - https://rb.gy/e154d1 Facebook - https://rb.gy/09d1b9 Twitter - https://rb.gy/e23220

Aidha amesema kwamba, atahakikisha rasmali za serikali zinawafikia wananchi na kutumika ipasavyo bila visa vyovyote vya ufisadi.

Rufftone ametoa ombi kwa wakazi wa kaunti ya Nairobi kumpigia kura na pia kudumisha amani na pia kupiga teke dondandugu la ukabila ambalo limekumba taifa hili kwa muda.