Kuhadaiwa ndani ya Uhusiano

Mchumba wangu kamleta chumbani mpenzi wake akidai ni jamaa yake

Ikawa sasa Isabel anadona pawili –hataki kumucha mpenzi wake mpya wala kumuacha yule Alfred ambaye walikuwa wamefufua mapenzi tena .

Muhtasari
  •  Msichana akajiona stadi kwamba ataweza kucheza  kama sogora na hivyo baada ya kwenda Mombasa wakaanza kuishi na Alfred katika nyumba  moja .
  • Yaani  walimwengu hawana stara ,peupe machoni unahadaiwa kimapenzi  bila kujua .

 

Alfred  Musambi alijiona mjinga wa shule lakini hakujua maisha yamemtayarishia mshutuko  wa kuonekana hata mjinga Zaidi .

  Mapenzi haya ya kuanzia shule ya upili kwake yalionekana kama yatakayodumu  na baada ya kupoteleana na Isabel wakati kila mmoja alipohamia mji mwingine baada ya  shule ya upili ,ilikuwa bahati sana walipopatana tena kupitia  mitandao ya kijamii . walipojikumbusha maisha yao ya shuleni kama wapenzi ,waliamua kuendeleza mambo walipoyaachia na  ndipo uamuzi wa   Isabel kuja kuishi nan a Alfred mjini Mombasa ulipozua makubwa .

 Isabel akahamia Mombasa kutoka  Wote ,huku akijua fika kwamba   uhusiano wake na  Alfred ulikuwa umepangwa tangu jadi na mola na utaishia  kuwa ndoa . Jambo ambalo hakuwa amejikumbusha ni kuhusu uhusiano wake na mwanamme mmoja wakati huo pale  Wote ambao hakuwa tayari kuusalimisha . Ikawa sasa Isabel anadona pawili –hataki kumucha mpenzi wake mpya wala kumuacha yule Alfred ambaye walikuwa wamefufua mapenzi tena .

 Msichana akajiona stadi kwamba ataweza kucheza  kama sogora na hivyo baada ya kwenda Mombasa wakaanza kuishi na Alfred katika nyumba  moja .Muda usio mrefu , mpenzi wake  Isabel  wa kutoka Wote anaye pia alisafiri kwenda Mombasa kuishi katika nyumba ile ile ,ikawa wamepanga njama ya kumdanganya Alfred kwamba walikuwa binamu kwamba mtu na Cousin yake sasa huwezo kuingilia wala kushuku lolote .

 Wakati Alfred alipokuwa amekwenda kazini ,aliwaacha chumbai pale mtu na mpenzi wake ambao walifanya yote waliotaka . Wakati mwingine mchana , yule mpenzi wa pili alikuwa akitoka kwenda mjini kutafuta kazi lakini   majirani waligundua mambo ya kushangaza kwa sababu walishuhudia kwamba Isabel alikuwa kaishi na wanaume wawili na mmoja hakuwa jamaa yake kama alivyodai kwa sababu mchana peupe walikuwa wakijifungia chumbani na kufanya mambo yao kabla Alfred hajarejea .

 Kwa sababu daku daku za baadhi ya majirani hazifichiki ,mmoja alipata ujasiri kwa kumuambia Alfred kuhusu kilichokuwa kikifanyika .Mtego uliwekwa na kama inavyotajiwa ,ilibainika wazi wazi kwamba mtu na cousin yake walikuwa ni Isabel na mpenzi wake ambao walikuwa wakimdoea Alfred kwa kuishi kwake ,kula vyake na kumhadaa ilhali walikuwa wakijua wanachofanya .

 Ilichukua nguvu za polisi  kuzuia maafa pale kwa sababu hasira za Alfred hazikuweza kutulizwa hata na majirani waliomtaka awe mtulivu wakati Isabel na ‘Cousin’ yake walipokuwa wakifungisha virago vyao kuondoka kutoka chumba chake . Yaani  walimwengu hawana stara ,peupe machoni unahadaiwa kimapenzi  bila kujua .

 Je,unawajua binamu za mpenzi wako? Chunga sana !