Makubwa haya

Nilipompata na kifaa cha ‘Vibrator’ nilijua uhusiano wetu ulikuwa umefika mwisho

Alice hakuwa na jibu wala hata hakujivurugia nguvu kwa kujitetea.

Muhtasari
  • Vitu ambavyo alikuwa akisikia na kuona mitandaoni sasa vilikuwa umbali wa mita mbili na alipoketi.
  • Yote yalianza siku moja alipokuwa katika chumba cha mpenziwe  akitafuta taulo ya kujipanguza maji alipotoka bafuni kisha ghafla akaona kifaa chenye mfano wa  uume.

 

Kuna sababu nyingi ambazo hufanya uhusiano kati ya wapenzi kufika tamati. Usaliti wa mpenzi wako kuwa na mwingine huumiza sana na huwa kibarua kwa watu wengi kujikwamua kutoka usaliti huo. Lakini utahisi vipi endapo utagundua kwamba mpenzi wa pembeni wa mwenzako sio mtu bali ni kifaa?

Hakuna kilichomtayarisha Francis kwa hisia alizopata wakati  alipogundua kwamba mpenzi wake wa  mwaka mmoja unusu Alice  alikuwa na kifaa maalum cha kujipa raha za kimwili yaani vibrator. Vitu ambavyo alikuwa akisikia na kuona mitandaoni sasa vilikuwa umbali wa mita mbili na alipoketi. Yote yalianza siku moja alipokuwa katika chumba cha mpenziwe  akitafuta taulo ya kujipanguza maji alipotoka bafuni kisha ghafla akaona kifaa chenye mfano wa  uume. Kwa sababu ya kutaka kujua kilikuwa cha kufanyia nini alikichukua na kukiangali kwa karibu. Makosa! hapo ndipo alipogundua kwamba kifaa kile kilikuwa  ni vibrator na kilikuwa na sehemu ya kuweka batari ndogo na nyaya za kukiunganisha kwa umeme.

Alipokiwasha  ili kuthibitisha hasa ni  kweli alichokuwa akiona, kiliwaka na kuzunguka kwa kasi iliyolenga kumpa raha na uhondo wote mtumiaji wake. Hasira zilimkomaa mwili mzima huku woga nao pia ukijikaribisha katika fikra zake. Alishindwa alie au  acheke kwani hapakuwa na siri kwamba  Alice alikuwa tayari amejenga mazoea na kukitumia kifaa kile na kulingana na jinsi alivyokiweka katika sehemu salama na kukifunika kwa kitambaa nadhifu, alikuwa ashajenga uhusiano wa karibu na vibrator ile.

Hakuna kitu ambacho humkwaza mwanamume kama kujua kwamba kazi yake muhimu sana imechukulia na mashine na  machungu hayo hayawezi kamweza kutulizwa na msamaha wa aina yoyote. Akiwa amejihami kwa ushahidi ule, Francis alijaribu kumkabili mpenzi wake akitaka maelezo kuhusu mbona alikuwa na vibrator chumbani. Alice hakuwa na jibu wala hata hakujivurugia nguvu kwa kujitetea. Alisalia kimya amesimama tisti  huku  akikosa hata lepe la  majuto mwake, jambo ambalo lilikuwa ujumbe tosha kwa Francis kwamba  hangeweza kamwe kumridhisha Alice jinsi alivyokuwa akiridhika na huduma na mzunguko wa kifaa kile. Kama  radi kighafla, uhusiano wao wa mwaka mmoja unusu na mipango yote iliyeyukia pale na ikawa bayana kwamba hakuna kati yao aliyekuwa tayari kutafuta suluhisho wala kuzungumzia  kiwango cha usaliti wa Alice kutumia  Vibrator kujiridhisha kingono.