Uaminifu katika Uhusiano

Unaweza kufanya kipi wakati mpenzio anakufuata kila uendapo?

Mambo yalizidi na kuwa mabaya wakati Willy alipoanza pia kuyafutilia mawasiliano yake kwenye simu akitaka kujua kila alichozungumza na mtu Fulani katika simu yake n ahata kusoma jumbe zote .

Muhtasari
  • ‘Angetokea tu hata wakati nipo darasani,ningetoka nje ili kuzungumza naye kisha angeniambia kwamba ananijulia hali  halafu tungeagana kisha aondoke’ anasema
  • Lakini alianza kupatwa na hofu wakati  Willy alipoanza kuja wakati wote n ahata siku nyingine angekuja pale shuleni Zaidi ya mara tatu kwa kisingizio cha kuja kumjulia hali

 

Wakati umetekwa na mapenzi huwezi kuona kasro katika mwenzio ,lakini baada ya kuzoeana kuna vitabia vya kutisha  ambavyo mwenzako huanza kuonyesha . amesimulia mwanadada mmoja kuhusu tabia ya kushangaza ya mpenzi wake ambaye alikuwa na mazoea ya kumfuata kokote alikokuwa akienda na baadaye ikabainika huenda alikuwa na tatizo la kisaikolojia ili kuweza kujua kila alihokuwa akifanya .

Beverlyn anasema mwanzoni alipokuwa kazini wakianza uhusiano na  Willy ,hakuna akilichoonekana kuwa cha kutisha kwani angekuja wakati wowote ghafla pale shule ambapo  Beverlyn alikuwa mwalimu .

‘Angetokea tu hata wakati nipo darasani,ningetoka nje ili kuzungumza naye kisha angeniambia kwamba ananijulia hali  halafu tungeagana kisha aondoke’ anasema

Lakini alianza kupatwa na hofu wakati  Willy alipoanza kuja wakati wote n ahata siku nyingine angekuja pale shuleni Zaidi ya mara tatu kwa kisingizio cha kuja kumjulia hali .Ni baadaye tu ndipo Beverlyn alipogundua kwamba mwenzake alikuwa na hofu ya kuachwa na hivyo basi kuna dhana aliokuwa nayo ya kutaka kujua kila alichokuwa akifanya akiwa kazini n ahata alianza kumuuliz amaswali kuhusu watu aliokuwa akizungumza nao pale shuleni .

Siku moja alijitosa ghafla katika mkutano wa walimu na wazazi akitaka kuzungumza na Beverlyn –kisa na maana? Alitaka kumjulia hali na hapo ndipo tofauti kati yao ilipoanza kuzuka . Bev alijaribu kumueleza kwamba ziara zake kuja pale kazini zilikuwa zikimvuruga na pia kumharibia mipangilio yake ya kazi lakini Willy alichukulia hilo vibaya akidai kwamba mpenzi wake alikuwa akimficha kitu na hakutaka aje shuleni kwa sababu alikuwa na uhusiano na mwalimu mwenzake pale shuleni .

Mambo yalizidi na kuwa mabaya wakati Willy alipoanza pia kuyafutilia mawasiliano yake kwenye simu akitaka kujua kila alichozungumza na mtu Fulani katika simu yake n ahata kusoma jumbe zote . Beverlyn alijuwa kuna tatizo wakati Willy  alipoichukua nambari ya mwalimu mkuu wa shule alikokuwa akifanya kazi na kumtumia ujumbe wa kumtisha kwamba aachane na Beverlyn. Ilikuwa wazi kwamba mwalimu alikuwa kajaiingiza katika uhusiano na ‘Psycho’.