Usaliti wa damu

Hata dadako ‘atakuvalisha kanzu’ kwa kukwepa na mumeo

Kinachompa wasi wasi Rachel ni kwamba Luis sasa anataka kuja kwao rasmi ili kujitambulisha kama mume wake

Muhtasari
  •  Anasema wakati Norah alipotengana na  mume wake  Luis ,ndipo walipoanza kuwasiliana baada ya kama mwaka mmoja hivi .
  • Sasa swali lake ni je,alifanya makosa? Kwa sababu baadhi ya watu wa familia wanahisi kwamba huenda ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya dadake.

Rachael  anataka majibu na mtazamo wa kumpa  utulivu wa kimawazo kwa sababu  amefanya jambo ambalo limeigawanya familia yake kati kati . Rachael  alianza kuishi na mume wa zamani wa dadake . Anasema hakuwahi kuwa katika uhusiani na  mume huyo wa dadake wakati alipokuw bado yupo katika ndoa na dadake mkubwa Norah .

 Anasema wakati Norah alipotengana na  mume wake  Luis ,ndipo walipoanza kuwasiliana baada ya kama mwaka mmoja hivi . Sasa swali lake ni je,alifanya makosa? Kwa sababu baadhi ya watu wa familia wanahisi kwamba huenda ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya dadake.

Rachael anajitetea  kwamba kabla ya   Luis kutengana na Norah hakuwahi kufikiria kwamba siku moja watajipata pamoja kama mke na mume lakini  amempenda baadaye wakati alipoachana na dadake .  Norah aliposikia kwamba mume wake wa zamani sasa analenga kumuoa rasmi dadake mdogo  ,amekasirika sana na hajakuwa akizungumza na Rachel kwa takriban miaka mitatu sasa . Kunao katika familia wanaohisi kwamba Rachel hafai kulaumiwa kwa sababu hata hakuwa nchini wakati Norah na Luis walipokutana na kuoana .

Kinachompa wasi wasi Rachel ni kwamba  Luis sasa anataka kuja kwao rasmi ili kujitambulisha kama mume wake .Lakini hilo haliwezi kufanyika wakati  mambo hayajawekwa wazi na kuzungumziwa kwa sababu kunao baadhi ya watu wa familia  yao ambao tayari wamesema hawatahudhuria hafla hiyo wala kumtambua Luis kama mume wa  Rachel kwa sababu alimpokonya dadake mume .

 Rachel hataki sifa hiyo ya kushtumiwa kama aliyevunja ndoa ya dadake ili kumchukua mume wake , kulingana naye ,sababu za ndoa ya dadake na Luis kuvunjika ni tofauti sana na wanachofikiria watu kwani kuna mengi ambayo jamaa na marafiki hawayajui lakini sasa atalazimika kuyasema peupe ili ulimwengu umpe nafasi ya kupumua na kundelea kujihisi kama mke wa mtu bila shutuma za kuwa ‘mwizi’ wa mume wa dadake.

 Je,inastahili kweli kujihusisha na mtu ambaye amekuwa ume au mke wa jamaa yako? Wengi wametoa maoni mbali mbali kuhusu hili lakini wanachokubaliana  watu wengi ni kwamba kama heshima kwa mtu wa familia yenu ambaye ameathiriwa na kuvunjika kwa uhusiano basi hufai kujihusisha tena na uhusiano ambao utamkumbusha mwenzake katika familia makovu ya kale . Kinachotisha hata Zaidi ni kwamba tayari Norah na Luis walikuwa na Mtoto mmoja ambaye sasa kando na kuwa atamuita Rachael kuwa shangazi yake ,pia atamtambua kama mamake wa kambo!