Kuacha watu Mataani

Nilivyosema naenda msalani na kukwepa sherehe ya kulipa mahari!

Hivyo ndivyo hafla nzima ilipozimwa na siku nyingine kupangwa uku watu wa akina msichana wakiwachwa vinywa wazi .

Muhtasari
  •    Ilipofika wakati wa mazungumzo kuhusu mahari sasa ,hapo ndipo Edward alipokata kauli mapema  kwamba yeye hatovumilia alichokiona kama unyanyasaji
  •  Wakati wa mapumziko kidogo katikati ya majadiliano ,Edward aliondoka bila hata kuwaambia watu walioandamana naye kwamba anaondoka

 

 

Edward  Kinza hakungoja kujionea  masaibu ya kutakiwa kulipa maeldu ya pesa kama faini kwa ‘makosa’ kadhaa wakati wa sherehe ya kulipa mahari ya mke wake .

 Anasema  kilichofaa  kuwa siku ya furaha na kumbukumbu kiligeuka kuwa siku ya kumpunja fedha kulingana naye kwa sababu ilikuwa imechukua muda mrefu yeye kutafuta fedha kidogo alizoweza kupata ili kwenda kutoa angalau kitu kidogo kwa akina mkewe . Walipofika kwa kina mkewe anasema palianza kuwekwa sheria na vikwazo vingi kuhusu ajambo moja hadi jingine na pale akina shangazi wakaanza kuandika chini faini ambazo angefaa kulipa kwa kutofanya hili au lile na mambo kama hayo .

   Ilipofika wakati wa mazungumzo kuhusu mahari sasa ,hapo ndipo Edward alipokata kauli mapema  kwamba yeye hatovumilia alichokiona kama unyanyasaji . Wazee ambao hakutaka hata kuwaangalia mara ya pili kutoka upande wa msichana walismama kidete kwamba lazima singetolewa shilingi laki nane kabla ya mazungumzo mengine kuhusu msichana wao yafanywe . Edward anasema alikuwa ameshamuambia mpenzi wake kuhusu hali yake ya kifedha na alijua kwamba mtoto wa watu angezungumza na jamaa zake walegeze kamba kidogo.

 Lakini ni kama ujumbe huo haukuwafikia kwa sababu siku ya siku ilipofika ,wakati wa kikao cha kuafikia kuhusu mahari ,wazee hao walisimam kidete na kudai kwanza pesa hizo zitolewe .Ujumbe wa Edward ulikuwa umejitayarisha na kitita cha shilingi laki mbili pekee na hawakuwa na budi ili kufadhaika na msimamo mkali wa baadhi ya wajomba na wazee kutoka upande wa msichana

 Edward na ujumbe wake walijaribu kuwaeleza wazee kwamba safari hiyo sio yao  ya mwisho na kwamba wangerejea tena baada ya muda  Fulani lakini  hakuna aliyewasikiza . Hapo ndipo Edward alifanya jambo ambalo wengi hawalifikiri angelifanya –Aliamua kujianzia mwendo na kuondoka!

 Wakati wa mapumziko kidogo katikati ya majadiliano ,Edward aliondoka bila hata kuwaambia watu walioandamana naye kwamba anaondoka .Alishika njia na kutembea kwa miguu hadi katika barabara kuu na kuchukua basi kurejea Nairobi kutoka Maragua . Simu nayo akazima na kuendelea na maisha yake .

 Juhudi za kumtafuta kwenye simu na kujaribu kuwashawishi baadhi ya jamaa zake wamrai arudi ziliambulia patupu kwani alihisi kutumiwa vibaya ama kupunjwa fedha zake wala hiyo haikuwa tena shehere ya kulipa mahari kwake bali ilikuwa ni kama kichinjio .Hivyo ndivyo hafla  nzima ilipozimwa na siku nyingine kupangwa uku watu wa akina msichana wakiwachwa vinywa wazi .