Kutumiwa vibaya

Sema Kukaangwa?Wakati mwingine unatumiwa kama kivuli..kisha unaachwa mataani!

Leonard hakuwa tayari kushauriwa . Uhusiano wao huo wa siri ulidumu kwa mwaka moja na hata wakati moja Leonard aliondoka kwake kuanza kuishi na Sheilla .

Muhtasari
  • Kila mtu ambaye hakuwa ameoa ama kuolewa alitaka kuwa katika ndoa kama ya  Leonard na Vickie .
  • Hata hivyo wanaume na tamaa zao hawatosheki wala kuona mbele .

Kuna msemo kwamba unavuna unachopanda . wengi hufikiria msemo huo unahusiana na mbegu au kilimo ,lakini smemo wenyewe ni kuhusu maisha na jinsi vitendo vyetu huturudi

 Hakuna anayefahamu  uhalisia wa msemo huo  vizuri kama  Leonard ambaye alimuacha mkewe wake wa miaka 7 ili kupata raha za mwanamke mwingine aliyeonekana mrembo Zaidi na  mwenye miondoko ya kisasa lakini matokeo yake yameishia kuwa kilio na majuto.

 Leonard alikuwa katika ndoa salama na yenye furaha na mke wake Vickie  na wengi katika familia na rafiki zao walikuwa wakiwatazama kama kilelezo kwa watu wa rika lao kwa sababu ya jinsi mapenzi yao yalivyokuwa na mvuto na uhalisia wa kutamaniwa na kila mmoja ,sio kazini ,kanisani na hata katika familia zao .

 Kila mtu ambaye hakuwa ameoa ama kuolewa alitaka kuwa katika ndoa kama ya  Leonard na Vickie . Hata hivyo wanaume na tamaa zao hawatosheki wala kuona mbele . raha za muda mfupi na  mvuto usiodumu umewafanya wengi kutupa bahati na hata kujiangamiza kwa maamuzi mabaya na hivyo ndivyo  jinsi  Leonard alivyojipata katika lindi la majuto .

 Yote yalianza wakati Leonard alipokutana na kipusa mmoja kazini kwake na wakati msichana huyo alipoletwa kutambulishwa ,  msimami wake Leonard alimpa jukumu la kuhakikisha kwamba mfanyikazi huyo mgeni Sheila anaelkezwa na kufunzwa baadhi ya kazi zake na Leonard . Ilikuwa rahisi kuanza mazoea na urafiki wao wa kazini ukajipata umegeuka kuwa jambo tofauti sana kwa mshangao wa watu wengi ambao walijua kwamba  Leonard alikuwa na mke na hakuwa na tabia za kuchimba huku na huku .

Muda haukudumu kabla ya Leonard kujipata kashafanya zinaa na Sheilla na licha ya onyo kutoka kwa wenzake kwamba anaiweka ndoa yake hatarini , Leonard  hakuwa tayari kushauriwa . Uhusiano wao huo wa siri ulidumu kwa mwaka moja na hata wakati moja Leonard aliondoka kwake kuanza kuishi na Sheilla .

 Ingedhaniwa kwamba safari yake hiyo mpya ingekuwa rahisi lakini hakujua yaliomngoja kwai muda haukudumu kabla ya Sheilla kuondoka naye baada ya kumpata mwanamme aliyemzidi umri na ambaye pesa zake hungeweza kuzihesabu hata kwa kikokoto. Sheilla aliacha kazi na ungemuona tu mitandaoni akiweka picha za safari anazofanya nje ya nchi na mpenzi wake ‘mzee’. Hivyo ndivyo adhabu kwa Leonard ilivuokuja na ikawa sasa safari ya kurejesha mkia nyuma na kumrudia mke wake ikaanza . Hakuna aliyetaka kumsikiza kwa sababu wakati aliposhauriwa kuhusu matokeo ya vitendo vyake ,aliona walimwengu wamejiingiza sana katika maisha yake na kumzuia kupata raha alizotaka  yeye .