Mahusiano

Nilimdanganya mimi ni shoga-Alitoroka usiku huo

Erica anasema tangia hapo mvulana huyo hakuwahi hata kumsalimia na kila alipomuona umbali wa mita kadhaa ,alipiga kona ili wasije wakakutana .

Muhtasari
  • Richard alimuambia mwanadada huyo kwamba yeye hakutaka uhusiano naye kwa sababu alikuwa mpenzi wa jinsia mmoja na alitaka tu mahusiano na wanaume wenzake
  • Sio Richard pekee aliyeitumia mbinu hiyo kujinasua bali kuna wanadada pia ambao hudanganya kwamba wao ni wapenzi wa jinsia moja ili kuwafukuza wanaume wanaowasumbua na kuwafuatafuata .

 

 

Kuna msemo kwamba kuna njia nyingi za kumuua  mende na kwa Richard  Ekuro msemo huo ulijitokeza  wazi wakati msichana mmoja waliyekuwa naye katika uhusiano alipokataa ‘Kuachika’.  Richard alikuwa amekutana naye na kutaka wakatize uhusiano wao kwa sababu kadhaa ambazo alimpa lakini mwanadada hakuonekana kutilia mkao wala kujali kuhusu uamuzi huo na wakati mwingi aliendelea kumtumia jumbe kama wanavyofanya wapenzi .

Baada ya kuwauliza rafiki zake wampe ushauri kuhusu anachofaa kufanya ili msichana huyo akome kumsumbua ,mmoja wao alimpa  wazo ambalo hadi leo wakikumbuka kicheko hutawala hewa kwa sababu ‘dawa’ hiyo ilifanya kazi   vizuri sana .

Richard alimuambia mwanadada huyo kwamba yeye hakutaka uhusiano naye kwa sababu alikuwa mpenzi wa jinsia mmoja na alitaka tu mahusiano na wanaume wenzake . Hilo lilimtoa mbuio mwanadada huyo asipate hata muda wa kuhoji iwapo alichokuwa akisema Richard kilikuwa cha kweli ama ni maigizo . Laiti angelijua kwamba ilikuwa mboni ya kumfukuza ,maskini hangeondoka mwanadada huyo lakini kufikia wakati alipogundua kwamba Richard alimchezea shere ,tayari kila mmoja wao alikuwa ashapiga hatua nyingine na maisha yake na hawangeweza kurudiana .

Zipo mbinu na wongo mbali mbali ambao wanaume wamezitumia na hata wanawake kuachana na wapenzi wao bila kuulizwa amswali mengi nah ii bila shaka ni mojawapo ya inayofanya kazi  haraka kuliko unavyotarajiwa . Sio Richard pekee aliyeitumia mbinu hiyo kujinasua bali kuna wanadada pia ambao hudanganya kwamba wao ni wapenzi wa jinsia moja ili kuwafukuza wanaume wanaowasumbua na kuwafuatafuata .Erica ,ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu jijini Nairobi ,anasema baada ya kusumbuliwa kwa Zaidi ya mwaka mmoja na mvulana mmopja waliyekuwa naye darasani ,siku moja alipata ujanja huo na kumdanganya kwamba yeye alikuwa tu akiwapenda wasichana  .

Erica anasema tangia hapo mvulana huyo hakuwahi hata kumsalimia na kila alipomuona umbali wa mita kadhaa ,alipiga kona ili wasije wakakutana . Anasema aliwashauri wenzake kuhusu ujanja huo na wengi wakajipata wanaitumia na kujiepusha na  sarakasi za watoto wa kiume kuwatongoza licha ya wao kujua kwamba walikuwa na mahusiano na wasichana wengine chuoni humo