Mafunzo kila mmoja anapaswa kujifunza kutokana na drama yake Samidoh

Muhtasari
  • Mafunzo kila mmoja anapaswa kujifunza kutokana na drama yake Samidoh
samidoh 3
samidoh 3

Msanii Samidoh wikendi iliyopita alivuma uku akivuma kwa siku kadhaa, hii ni baada ya mwanasiasa Karen Nyamu kufichua ni baba wa mtoto wake.

Karen akiwa kwenye mahojiano alisema kwamba hajua kama msanii huyo alikuwa ameoa.

KUpitika kwenye ukurasa wake Samidoh wa instagram aliomba mkewe msamaha, huku Karen pia akiomba mkewe Samidoh msamaha.

Lakini je tunapaswa kujifunza nini kutokana na hayo yote, kuwa na mtoto nje ya ndoa na mambo mengi.

Haya hapa mafunzo ambayo tunapaswa kujifunza kutokana na drama ya wawili hao;

1.Endelea na maisha

Ndio kama kosa limetendeka limeshaa tendeka kwa hivyo hamna haja ya kukaa au kujifungia kwa chumba chako na kulia siku kadhaa.

2.Ni siku mpya

Jambo ndio lilitendeka leo lakini haupaswi kuamka siku ifuatayo ukiwa umekasirika kwa ajili ya yale yalitendeka jana

Ni siku nyingine na mpya kwa hivyo tengeneza maisha yako kutokana na makosa yako.

3.Sisi sote huwa tunakosa

Hamna mtu ambaye anaweza sema kwamba ni mtakatifu na hajawahi fanya kosa, lkini ukijipata katika hali hiyo jua mtu hukosa na kosa si kosa likirudiwa ndio kosa.

4.Omba msamaha

Kama ni wewe kuwa mjasiri kama Samidoh na uombe msamaha kwa unyenyekevu na wala si kujipiga kifua na kusema hamna mahali watu watakupeleka.

5.Ni vyema kusema ukweli kwa wapenzi wako

Haya kama mwanamume umeenda nje na kisha ukajipata na mtoto nje ya ndoa ambia mpenzi wako, na uweke mambo wazi yasije kupata mke wako kama hayuko tayari.

6.Makosa yakko hayakutambulishi

Ukifanya haitajiandika kwenye uso wako kwamba ulitenda kosa ili na lile, lakini cha muhimu rekebisha makosa yako