Orodha ya vipusa mashuhuri mwaka wa 2021 walio na chini ya miaka 25 wanaowakosesha wanaume usingizi

Muhtasari
  • Orodha ya vipusa mashuhuri mwaka wa 2021 walio na chini ya miaka 25
  • Baadhi ya vipusa hao wanawakosesha wanaume wengi nchini usingi kwa ajili ya urembo wao
Azziad Nasenya
Azziad Nasenya

Tasnia ya watu mashuhuri,inaendelea kukua kila kuchao huku baadhi ya watu mashuhuri wakizeeka na kujiondoa katika tasnia hiyo.

Wanaoendeleza tasnia hiyo ni vijana wenye nguvu, bidii,wachangamfu na hata wenye urembo wa kupindukia.

Baadhi ya vipusa hao wanawakosesha wanaume wengi nchini usingi kwa ajili ya urembo wao.

 

Makala haya tutaangazia vipusa ambao hawajafikisha miaka 25, bali wanafahamika sana katika tasnia ya watu mashuhuri.

Hii hapa orodha ya baadhi ya vipusa hai.

1.Gloria Kyallo

Ni dada yake mwanabiashara Betty Kyallo, Gloria ana urembo wa kupigiwa mfano na kipekee, kipusa huyo ana miaka  20.

2.Celestine Gachui

Anafahamika sana kama Selina kupitia kwa kipindi cha selina kinachopeperushwa jumatatu hadi ijumaa katika runinga ya Maisha Magic East.

Licha ya Gachui kuwa muigizaji pia ni msanii wa nyimbo za injili.

 
 

3.Azziad Nasenya

Alifahamika sana baada ya kufanya 'challenge' ya kibao chake msanii Femi One na Mejja cha 'utawezana'

Baada ya kupata umaarufu, alianza kuigiza katika kipindi cha selina, huku akifahamika siku moja baada ya nyingine.

Amekuwa akifanya 'chellenge' hizo kwa muda.

4.Rue Baby

Ni mwanawe msanii esther Akoth almaarufu Akothee,Rue ameingia katika tasnia ya watu mashuhuri huku akifahamika siku baada ya nyingine.

5.Shakilla

Ni mwanasosholaiti chipukizi ambaye alivuma kwa muda, baada yake kufichua mambo kadha wa kadha.

Licha yake kuvuma kwa mambo yote mabaya Shakilla ameonyesha ujasiri wake katika tasnia hiyo.