Najutia kumchukua mwanamume wa wenyewe-Mwanamke ajuta

Muhtasari
  • Katika maisha kila mtu lazima awe na majuto ambayo alifanya uamuzi kwa ajili ya jambo moja au lingine
  • Kuna wale huwa wanajiukumu kwa kile wanafanya ama walifanya na kuwa na majuto
  • Mwanamke mmoja alijutia kumchukua mwanamume wa rafikiye, ambaye alimuacha baada ya kumpa kifungua mimba wake
sad woman
sad woman

Katika maisha kila mtu lazima awe na majuto ambayo alifanya uamuzi kwa ajili ya jambo moja au lingine.

Kuna wale huwa wanajiukumu kwa kile wanafanya ama walifanya na kuwa na majuto.

Mwanamke mmoja alijutia kumchukua mwanamume wa rafikiye, ambaye alimuacha baada ya kumpa kifungua mimba wake.

"Tulikuwa tumeenda sherehe na rafiki yangu, alinitambulisha kwa mumewe, lakini kutooka siku hiyo tulipendana na mumewe

Tulibadilishana namba za simu na baada ya miezi miwili tulianza uhusiano wetu wa kimapenzi, wakati huo sikujali kile rafiki yangu alikuwa anapitia kwani mapenzi yalikuwa yananoga

Kwa sasa najuta sana kumchukua mumewe kwani alinipa mtoto kisha akanitoroka, sitawahi tamani kumchukua mwanamume wa mtu," Alieleza Mwanamke huyo.

Je ni jambo lipi ambalo unajuta kutenda na kufanya maishani mwako?