Ishara zinazoonyesha kwamba mtu anakufuata kwa karibu

Muhtasari
  • Ishara zinazoonyesha kwamba mtu anakufuata kwa karibu
  • Kwa hivyo kile kinachoweza kuanza kama hamu kubwa kwako inaweza kubadilika haraka kuwa hali mbaya
stalker-new-cbs
stalker-new-cbs

Licha ya kile unaweza kufikiria, sio lazima uwe mtu mashuhuri kuwa na mtu anayemfuatilia. Mara nyingi, watu hao tunawajua vyema, kama mwenzako au mwenza wa zamani.

Kwa hivyo kile kinachoweza kuanza kama hamu kubwa kwako inaweza kubadilika haraka kuwa hali mbaya, kwani wanakuwa watawala juu ya maisha yako.

Lakini ikiwa unaweza kuchukua ishara mapema vya kutosha, unaweza kujifunza jinsi ya kuzuia aina hizi za watu na kuendelea na maisha yako.

Ishara hizo ni kama;

1.Kuona mtu huyo huyo  mahali pamoja

Unamuona kila wakati akizunguka bila ya kufanya kazi yeyote, bali tu anakuchungua na kufuatilia maisha yako.

2.Kujua mengi kukuhusu kulio yale umewaambia

Kuna watu ambao wanatabia ya kuchunguza maisha ya watu na kuwafuatili kwa ukaribu, na kujua au kufahamu, mambo mengi kuliko yale umewaambia kuhusu maisha yako.

3.Kupigia na kuwasiliana na familia yako na marafiki zako

Kama mtu anataka kukufuata kwa karibu atawasiliana na familia au rafiki zao ili kujua ratiba yako ya siku hiyo, ili ajue mahali utakuwa kwa masaa fulani.

4.Kuja kukusaidia kila wakati, wakati wa jambo la dharura

Je anafahamu aje kila wakati ambapo umepatwa na dharura kwamba unahitaji msaada wake, hayo yana maana kuwa anakufuatilia kwa karibu sana.

Je wajua kwamba kuna mtu anakufuata kwa ukaribu? au umewahi fuata mtu kwa ukaribu.Kuna wale watakufuata kwa ukaribu kwenye mitandao ya kijamii na wale watakufuata kila mahali uendapo.