Ukiwa mtu mashuhuri lazima ufanye mambo yako kwa utaratibu, uili usijipate upande mbaya na wanamitandao.
Ndio kuna watu ambao huvaa suti lakini, hawajui kwamba haziwatoi vyema.
Lakini kuna baadhi ya wanaume mashuhuri Afrika ambao huvalia suti na kuwakosesha wanawake usingizi.
Katika makala haya tutazingatia wasanii ambao wakiwa na suti kila mwanamke atammezea mate.
1.King Kaka
Ni msanii kutoka nchini kenya na ambaye anapendwa sana na mashabiki wake kwa ajili ya kazi yake.
Msanii huyo akivalia suti kwa kweli wanawake wengi hukosa usinginzi.
2.Diamond Platnumz
Ni staa wa bongo kutoka Tanzania na ambaye anafahamika Afrika kote, Diamond amekuwa akitoa kibao kimoja baada ya kingine huku akiwashirikisha wasanii tofauti.
Staa huyo akivalia suti, huwa nakaa vyema na kufanya baadhi ya wanawake kummezea mate.
3.Bahati
Safari ya usanii ya msanii huyo inafahamika sana, kwani alifahamika sana kupitia kwa kibao chake cha 'mama' pia akivalia suti hutokelezea na kuwamaliza wengi.
4.Willy Paul
ni msanii ambaye huwa na msimamo wake, na ambaye hatafuti kiki kutoka kw mashabiki kwani anajua bidii ya kazi yake.
5.Rayvanny
Licha ya msanii huyo kuwa na drama nyingi katika maisha yake pia ukaa vyema akivalia suti
6.Jose Chameleone
Alivuma sana kwa ajili ya nyimbo zake, ni msanii kutoka Uganda na ambaye anapendwa sana na wanamitandao.
Ni miongonni mwa wasanii ambao wakivalia suti wanakaa vyema.