Wanawake!Ishara zinazoonyesha kwamba wewe sio mpenzi mkuu katika uhusiano wako

Muhtasari
  • Sijui nikuambie nini, ni jambo ambalo linasikitisha endapo utafahamu ukweli wa uhusiano wako wa kimapenzi
  • Umejikwaa kwenye ishara wewe ni mpango wa kando au vile husema kwa kimomba 'Side chick' wa pembeni

Sijui nikuambie nini, ni jambo ambalo linasikitisha endapo utafahamu ukweli wa uhusiano wako wa kimapenzi.

Umejikwaa kwenye ishara wewe ni mpango wa kando au vile husema kwa kimomba 'Side chick' wa pembeni.

Pamoja na mitandao ya kijamii na hofu ya kukosa, watu wanaogopa kujitolea kwa mtu kwa sababu wanafikiria kitu bora kitakuja.

Sasa, hii sio kisingizio kwa mwanamume kuwa kwenye uhusiano na kuwa na 'side chick' wa pembeni pia.

Wanajua lililo sawa na lipi baya Ikiwa wana marafiki wa kike wengi sio shida yako.

Kweli, kwa kweli, ni kidogo kwa sababu unaweza kuwa 'side chick'. Ikiwa una hisia za kushangaza juu ya uhusiano na hisia kwamba haimarishi chochote kati yenu, basi unaweza kuwa mpango wake wa kando.

Lakini hebu tusiruke kwa mawazo. Badala yake, hebu tuangalie ishara na kuweka vipande vya fumbo pamoja. Je! Wewe ni msichana wake mkuu au side chick?

Hizi hapa baadhi ya ishara hizo;

1.Muda mdogo na wewe

Utampata mwanamume huyo ana muuda mdogo na wewe endapo mtapatana, hata kama mmesema kuwa mnatenga muda huo kuwa pamoja.

2.Hatakutambulisha kwa marafiki zake au jamaa zake

Ni matamanio ya kila mwanamke mpenzi wake kumuonyesha watu wa kwao na hata marafiki zake, haya basi kaa macho, kama mpenzi wako hajakuonyesha rafiki yake mmoja, jua wewe ni 'side chick' na anakutumia tu.

3.Yuko kwenye simu yake kila wakati

Mkipatana kila saa na kila sekunde yuko kwenye simu yake, na wala hujawahi shika simu yake, wewe basi sio mpenzi wake, dada yangu na kwambia anza mbio za kutoka kwenye uhusiano huo kwa mapema.

4.Hata kupakia kwenye mitandao ya kijamii

Kwa maana anajua mpenzi wake atakuona akikupakia, hatakuambia chochote haswa kama unasheherekea siku yako ya kuzaliwa au siku yeyote maalum,hatafanya chochote.

Swali kuu ni kuwa ni lini wanaume wataona maana ya uhusiano wa kimapenzi na kuacha kuchezea hisia za wanawake?