Niliachana na mke wangu baada ya kupeleka pesa zake kwa mganga-Asema mwanamume

Muhtasari
  • Kuna wale huwa wanaachana kwa sababu tofauti, na wengine kwa ajili ya shinikizo kutoka kwa familia
  •  
    Bajeti ya nyumbani ikidhoofika mbona wanawake wengi hubadilisha tabia zao na kununa kila mara?
  • Nani anapaswa kulaumiwa bajeti ya nyumbani ikidhoofika ni mwanamume au mwanamke?

Ni sawali ambalo wanaume na wanawake wengi hupokea endapo amefichua kwamba waliachana na mpenzi wao.

Kwanini mliachana na ke wako au mume wako?

Kuna wale huwa wanaachana kwa sababu tofauti, na wengine kwa ajili ya shinikizo kutoka kwa familia.

Lakini mwanamume mmoja hakuwa tu na sababu kubwa bali aliachana na mkewe kwa ajili alipeleka pesa zake kwa mganga.

Bajeti ya nyumbani ikidhoofika mbona wanawake wengi hubadilisha tabia zao na kununa kila mara?

Nani anapaswa kulaumiwa bajeti ya nyumbani ikidhoofika ni mwanamume au mwanamke?

Au wanawake wa aina hiyo huwa wanatimiza msemo wa mkono mtupu haulambwi? sasa ni kazi ya jukumu la wanaume kujikakamua ili wasipate madharau kutoka kwa wanawake wao.

Huu hapa usimulizi wa mwanamume akipeana sababu aliachana na mke wake mapema mwaka huu.

"Nilikuwa najukumikia kila kitu kwa nyumba na hata kulia kodi ya nyumba, licha ya hayo yote mke wangu alikuwa ananiitisha pesa na alikuwa anafanya kazi

Pia nilikuwa nasadia familia yao, hata hivyo akipokea mshahara wake alikuwa anapeleka kwa waganga bila ya kushughulikia chcochote nyumbani

Nilihisi mambo yamefika mwisho tukaachana, nikamwambia aendelee kumpelekea mganga pesa zake," Alisema mwanamume huyo.