Orodha ya watu ambao hawapaswi kutoa maoni kuhusu ndoa yako

Muhtasari
  • Orodha ya watu ambao hawapaswi kutoa maoni kuhusu ndoa yako

Je! Unapanga kuoa au kuolewa?Inashauriwa sana kutafuta mapendekezo ya watu wengine, hata hivyo, hawapaswi kuamua nini kitakachoendelea katika ndoa yako au harusi.

Hii hapa orodha ya watu ambao hawapaswi kutoa maoni yeyote kuhusundoa yako.

1.Mitandao ya kijamii

Kuna baadhi ya wanandoa ambao wanamazoea ya kupakia viideo kwenye mitandao ya kijamii na kuonyesha jinsi wanaishi maisha yao.

Pia wamekuwa waathiriwa wakubwa wa jinsi wanamitandao wamekuwa wakisema kuhusu ndoa yao huku wengi wakiachana kwa ajili ya mitandao ya kijamii

Sio kila mtu ambaye yuko mitandaoni anakutakia mema katika maisha yako,hupaswi kuruhusu mitandao ya kijamii kuamua au kutoa maoni kuhusu ndoa yako.

2.Wazazi

Kuna baadhi ya wazazi ambao wanapenda kujihusisha na ndoa za watoto wao bila ya kujua kwamba wanaendelea kubomoa boma zao.

Kama unataka ndoa yako kudumu haya basi sio kila maoni ya mzazi wako unatilia maanani.

3.Marafiki

Sio marafiki wote ambao wanaheka na wewe wanakutakia mafanikio katika ndoa yako, pia jua yale ya kuwaambia marafiki zako kuhusu ndoa yako, na wala usitoe siri yako ya ndoa nje.

4.Baba wako wa kiroho

Ata baada ya kudhulumiwa katika ndoa yako, baba yako wa kiroho atataka tu ukae katika ndoa yako kwani hatatamani kuona umetenganaa na mke wako au mume wako.

Ulingana na maoni yangu wewe mwenyewe ndiye unapaswa kuamua jinsi ndoa yako itaendelea na jinsi mtakavyo kuwa pamoja kama una furaha.