Ishara zinazoonyesha hauko tayari kuwa katika uhusiano mwingine

Muhtasari
  • Ishara zinazoonyesha huyuko tayari kuwa katika uhusiano mwingine
long distance lovers
long distance lovers

Wengi wetu tunataka uhusiano lakini kwa kiwango cha ufahamu, hatuyuko tayari kwa uhusiano mzito hata ikiwa unajisikia uko tayari.

Kuna wale hujihusish katika uhusiano wa kimapenzi kisha baada ya siku chache wanaachana kwa jambo ndogo, kwani hakuwa tayari kuwa katik auhusiano.

Hizi hapa ishara zinazoonyesha kwamba huyuko tayari kuwa katika uhusiano wa kimapenzi licha yako kuhisi kwamba unataka kuwa katika uhusiano mwingine.

1.Una Mahitaji makubwa kwa Mwenzako

Viwango ni nzuri lakini watu ambao hawayuko tayari kwa uhusiano mara nyingi huwa na orodha ndefu ya vitu wanavyotamani kutoka kwa mwenzi wake.

Mara nyingi watakua na watapata kosa kwa mwenzi wao.

2.Unafurahishwa na drama

Kwenye kiwango cha fahamu, unafurahishwa na wanaume wenye machafuko na hawapatikani. 

Kama unapendezwa na wanaume ambao wako na familia haya basi fahamu kwamba hauyuko tayari kuwa katika uhusiano wa kimapenzi.

3.HUjamsahau aliyekuwa mpenzi wako

Kama kila wakati unamfikiria aliyekuwa mpenzi wako baada ya kuachana jua na ufahamu vyema kwamba huyuko tayari kuwa katika uhusiano mwingine kwa hivyo haupaswi kufikiria kujihusisha na uhusian mwingine kwani utakuwa uanachezea hisia za mwenzako.

4.Huna furaha na wewe mwenyewe

Kabla ya kujihusisha katika uhusiano mwngine unapaswa kuwa na furaha na kisha ujipende, kama hayo yote huna jua kwamba si vyema kujihusisha na uhusiano mwingine.