Collabo kati ya Diamond na Wiz Khalifa itabadilisha muziki wa Afrika Mashariki?

Muhtasari
  • Collabo kati ya Diamond na Wiz Khalifa itabadilisha muziki wa Afrika Mashariki?
Diamond Platnumz na Wiz Khalifa
Diamond Platnumz na Wiz Khalifa
Image: Instagram

Msanii nyota wa bongo Tanzania Diamond Platinumz ndiye msanii wa muziki aliyefanikiwa zaidi kutoka Afrika Mashariki na Kati.

Msanii uyo anafahamika sana kupitia kwenye bidii ya kazi yake na jinsi amekuwa akiwashirikisha wasanii tofauti katika muziki wake.

Njia yake ya muziki inaonekana kuwa ya kirafiki kwani amejihusisha na marafiki na familia yake kwa pamoja.

Muziki wake umeweza kuvutia kizazi cha wazee na kizazi kipya.Kweli utashangaa kupata mtoto wa miaka mitano akiimba wimbo wa Diamond barani Afrika.

Kimataifa, Diamond ameunda mtandao mkubwa wa wasanii na wapenzi wa muziki wake huku akitafuta kutambuliwa katika kiwango cha ulimwengu.

Diamond ameteuliwa na kutuzwa tuzo tofauti za muziki, licha ya changamoto za muziki msanii huyo hajaweza kufa moyo amezidi kutia bidii katika kazi yake ya usanii.

Ingawa amefanya ushirikiano na wasanii wa Amerika kama Ripiki Rick Ross, wasanii wa RNB Ne-Yo na Omarion, naamini ushirikiano wake na msanii wa nyimbo za hiphop wa Amerika Wiz Khalifa utakuwa mzuri na utabadilisha muziki wa Afrika mashariki.

Wiz Khalifa ametengeneza muziki bora kabisa kuwahi kusikika katika historia ya muziki wa hip hop ulimwenguni kote.

Ana sifa za kupata wataamaji  bilioni kwenye YouTube kwenye wimbo wake wa See You Again.

Ushirikiano wao ungeweza kuona Diamond Platinumz akpata watazamaji wa kiwango cha bilioni wakati wowote kwani Afrika anasikilizwa vizuri.

Swali kuu ni je collabo kati ya wasanii hao wawili itaweza au haitaweza, na je itabadili muziki wa Afrika Mashariki?