Haya hapa mambo ambayo hukuyafahamu kuhusu Caroline Kangogo

Muhtasari
  • Haya hapa mambo ambayo hukuyafahamu kuhusu Caroline Kangogo
Image: HISANI

Baada ya taarifa kuenea kwamba afisa mtoro Caroline Kangogo amefariki dunia, maswali mengi yameibuka miongoni mwa Wakenya.

Kangogo alipatikana ameaga dunia Ijumaa, Julai 16 nyumbani kwao Elgeyo Marakwet baada ya kutoweka tangu Julai 5.

Baada ya kutangazwa kwa kifo chake, Wakenya walifurika mitandaoni kutoa maoni yao kuhusiana na hisia zao.

Kangogo aligonga vichwa vya habari baada ya kumuua polisi mwenzake,katika hali isiyojulikana.

Haya hapa mambo ambayo hukujua kuhusu Caroline Kangogo;

Caroline amezaliwa Elgeyo Marakwet.

Koplo Kangogo alikuwa akihusishwa na mauaji mawili, alimpiga risasi polisi John Ogweno na mwanamume aliyefahamika kama Peter Njiiru.

Alisafiri kutoka Nakuru kwenda Thika kutekeleza mauaji ya pili.

Alikuwa na umri wa miaka 34.

Caroline alikuwa mama wa watoto wawili.

Alianza kufanya kazi katika kituo cha Polisi cha Nakuru mnamo 2015 hadi kifo chake.

Alijiunga na jeshi la polisi mnamo 5/8/2008.