Ishara zinazoonyesha unamchumbia mwanamume mzuri

Muhtasari
  • Ishara zinazoonyesha unamchumbia mwanamume mzuri

Katika nchi au dunia ambayo imejaa 'mafisi' katika lugha ya mtaa, ni vigumu sana kutambua mwanamume mzuri na ambaye hatavunja moyo wako.

Lakini kunao wanawake wana bahati mzuri kwani hawajawahi patana na wanaume ambao wana nia mbaya maishani mwao au kuvunjwa moyo.

Kama mwanamke umempata mwanammume na unasema kwamba huyo ndiye ilhali hujui kwamba ni mwanamume mzuri, husitie shaka kwani hizi hapa ishara zinazoonyesha huyo ni mwanamume mzuri.

1.Anakukubali jinsi ulivyo

Katika uhusiano wa kimapenzi menzi wako anapaswa kukubali jinsi ulivyo, je na maanisha nini nikisema hayo, kama unabadilisa maisha yako au mavazi yako ili kumpendeza mpenzi wako jua huyo sio wako aua mwanamume mzuri kwako.

2.Ni mwaminifu

Ata akiambiwa na watu au marafiki mabaya kukuhusu mpenzi wako anapaswa kukuamini na yale umempa hata kama hayaendanishi na yale ameambiwa kukuhusu.

3.Anataka ushinde

Mpenzi mzuri atakutaka ushinde na anafurahi kwa dhati kwako unapopandishwa cheo, upandishwe mshahara na ushindi mwingine.

4. Unahisi upendo

Wanaonyesha mapenzi yao kila mara kwa kutumia lugha yao ya mapenzi. Wanajitahidi pia kukupenda jinsi unavyotaka kupendwa

5.Unamwamini

Katika kila uhusiano uaminifu ni jambo la maana sana, kwani ukiwa umemuamini mpenzi wako hamna kitu chochote kitawatenganisha.

6.Anakusikiza

Kuna baadi ya wanaume au wanawake hawana muda wa kuwasikiza wenzi wao, wanataka tu wao wasikizwe hata kama hawana shida yeyote.

Lakini ukimpata mwanamume ambaye anakusikiza haya basi fahamu kwamba huyo ni wako na ni mzuri.