Mume wangu aliniacha baada ya kujifungua mapacha,alileta mpango wake wa kando nyumbani-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Sio mmoja au wawili bali baadhi ya wanawake wengi hupita changamoto nyingi katia ndoa zao,hasa baada ya kujifungua
black-woman-crying-
black-woman-crying-

Sio mmoja au wawili bali baadhi ya wanawake wengi hupita changamoto nyingi katia ndoa zao,hasa baada ya kujifungua.

Nikiwa katika ziara zangu mwanamke aliyefahamika kama Josephine alinisimulia jinsi waliachana na mume wake baada ya kujifungua mapacha.

Ni furaha ya kila mume kukaribisha baraka katika ndoa yake, lakini mume wake Josephine alitupilia mbali baraka zake.

Huu hapa usimulizi wake;

"Baada ya kuwa kwa ndoa kwa miaka sita, nilibarikiwa na mapacha watatu, tabia za mume wangu zuzlianza kubadilika kila kuchao

Nilifanya kila niwezalo ili kumpendeza na kila niwezalo ili awapende watoto wetu lakini nguvu zangu ziliambulia patupu kwani alikuwa amebalisha mawazo yake kuhusu ndoa yetu

Baada ya miezi tano, alimleta mpango wake wa kando nyumbani na kisha akanifukuza nikiwa na watoto wangu

Miaka tano sasa imepita, sijui anaendelea aje wala hawahi nijulia hali baada ya kunitupa nje na watoto wangu usiku wa manane

Sijui nifanyeje,licha ya hayo yote ninampenda na roho yangu yote," Josephine aliongea.

Je ni ushauri upi unaweza kumpa mwanamke huyo?