Watu maarufu ambao walifunguka juu ya uhusiano wao wa kimapenzi 2021

Muhtasari
  • Tangu mwaka uanze, kuna mambo mengi ambayo yametokea katika mitandao ya kijamii
  • Tumeona watu mashuhuri wakituhumiwa kujihusisha na mambo haramu, wengine wakianza uhusiano mpya
Lilian Ng'ang'a na Juliani
Image: Boniface Mwangi/Twitter

Tangu mwaka uanze, kuna mambo mengi ambayo yametokea katika mitandao ya kijamii.

Tumeona watu mashuhuri wakituhumiwa kujihusisha na mambo haramu, wengine wakianza uhusiano mpya, wakati wengine kama mwanamuziki wa Tanzania Harmonize akitupwa na wapenzi wao.

Katika makala haya , tutaangalia watu mashuhuri wetu tunaowapenda ambao walifichua  kwa umma kwamba walikuwa wameanzisha uhusiano mpya.

Mastaa hao ni pamoja na;

1.Nadia Mukami na Arrow Bwoy

Nadia Mukami, ambaye kwa muda mrefu tangu aingie kwenye muziki alisisitiza kwamba amekuwa hajaolewa kila siku, hivi karibuni aliwashangaza mashabiki wake baada ya kubaini kuwa yuko kwenye uhusiano na mwanamuziki mwenzake Arroy Bwoy.

“Tunachumbiana? Ndio. Nimekuwa mpenzi wa Arrow / Ali kwa muda sasa. Nimekuwa nikichumbiana. Tumekuwa pamoja kwa muda mrefu kuliko vile watu wanaweza kudhani.

2.Rayvanny na Paula Kajala

Rayvanny alithibitisha uhusiano wao katika chapisho la Instagram. Mwimbaji alishiriki picha akiwa amemkumbatia Paula, na wote wawili wakitazama nje kupitia dirishani.

Kwenye ukurasa wake, Paula alishiriki picha hiyo hiyo na kuiandika kwa upendo.

Tangu kuthibitisha uhusiano huo, wawili hao wameonekana hadharani wakifurahiya maisha yao ya mapenzi pamoja.

3.Juliana na LIlian Ng'ang'a

Miezi kadhaa baada ya kudhaniwa kuwa Julius Owino, jina jingine Juliani na Lilian Ng'ang'a, mke wa zamani wa Gavana wa Machakos Alfred Mutua, walikuwa katika uhusiano, mwimbaji huyo amejitokeza kudhibitisha kuwa kweli wao ni kitu kimoja.

4.Ronald Ndubi na Dore Chege

Aliyekuwa muigizaji wa kipindi cha Maria Victoe, akiwa kwenye mahojiano alithibitisha kwamba yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na muigizaji mwenzake maggie.

Pia alifichua kwamba harusi iko njiani.