Fahamu kwanini waliokuwa wanandoa hurudiana baada ya muda

Muhtasari

•Moja wapo ya msingi katika kuingia tena kwenye uhusiano wa zamani ni kwamba unafahamu fika unachojiingiza ndani yake.

•Faida moja ya kurudiana na mpenzi wako wa zamani ni ufahamu wa kile kilichobadilishwa kwa wakati ambao mmekuwa mbalimbali.

•Kuhisi kuwa utakabiliwa na maumivu yale yale tena, kunaweza kukupa mtazamo wa mapema ili kuepuka maafa sawa na yaliyotokea awali.

Image: GETTY IMAGES

Mapema msimu huu, miaka 17 baada ya kutengana, Jennifer Lopez na Ben Affleck walirudiana - na kusababisha gumzo kubwa mtandaoni kuhusu kumbukumbu ya mapema miaka ya 2000, watu mashuhuri na uchambuzi wa kitamaduni.

Ni wanandoa wanaopendana kiasi kwamba wanafuatiliwa na wengi katika mitandao ya jamii kama Twitter.

Lakini pengine sababu inayosadikika zaidi na kuvutia sana watu wa kawaida na ni uvumi kwamba watu waliokuwa mashuhuri zamani wamepata tena upendo tena.

Kwa wengi, kurejea kwa upendo kwa wenzi wa zamani ni mapenzi ya kweli.

Ukweli huo unaweza kuwa hasi - wenye kujumuisha simulizi za tahadhari kati yao lakini kujenga uhusiano pia inaweza kuwa suala muhimu kulijaribu na pia lengo kwa watu wengine, haswa wakati hadithi za mafanikio zinasikika zikihadithiwa.

Kwa kuongezea, utafiti unaonesha idadi ya wanandoa ambao huachana na kurudiana ni ya juu kiasi cha asilimia 50.

Janga la corona nalo limeongeza kasi ya mchakato huu kwa wengine: katikati ya tatizo kubwa la kiafya na upweke, kutokujali ngono, watu wengi walijikuta wakianza kuwasiliana tena na wapenzi wao wa zamani, wakitumaini kupata cheche za mapenzi zile za zamani.

Wataalamu wanasema kwamba, ikiwa wenzi wote wa zamani wana shauku ya kurejea katika mahusiano, kuwavutia wenzi wao kunaweza kuwa na faida - ikiwa wako tayari kuweka juhudi.

Kipi kinachochochea waliotengana kurudiana?

Moja wapo ya msingi katika kuingia tena kwenye uhusiano wa zamani ni kwamba unafahamu fika unachojiingiza ndani yake.

"Kunaweza kuwa na faida za kweli kumjua mwenzi wako vizuri kabla ya kujaribu tena kudumisha uhusiano wa muda mrefu," anasema Michael McNulty, mtaalamu wa masuala ya wanandoa huko Chicago na mkufunzi katika Taasisi ya Gottman, shirika linalochunguza uhusiano na kutoa ushauri.

McNulty anasema kila uhusiano wa kimapenzi una "tofauti za kila wakati".

Hizi ni sehemu za mizozo inayoweza kutokea kama vile kuishi pamoja, pesa, ngono, watoto, marafiki, familia na mengine mengi.

Hata wenzi wenye furaha wanakumbana na changamoto hizo kwani uhusiano daima ni watu wawili tofauti na haiba tofauti na wenye mitazamo tofauti vilevile.

Kurekebisha mapenzi ya zamani hakika sio kwa kila mtu, wataalam wa uhusiano wanasema, lakini kujuana kwa awali kunaweza kusababisha kufaidika kwa kila mmoja wetu.
Kurekebisha mapenzi ya zamani hakika sio kwa kila mtu, wataalam wa uhusiano wanasema, lakini kujuana kwa awali kunaweza kusababisha kufaidika kwa kila mmoja wetu.
Image: GETTY IMAGES

McNulty anasema, kulingana na utafiti wa Taasisi ya Gottman, tofauti hizi za kudumu huchangia asilimia 69 ya shida za wanandoa wanazokabiliana nazo katika uhusiano.

Maswala yanayodumu kwa muda mrefu, yale yanayochipuka polepole ndio sumu kubwa katika uhusiano - wala sio tatizo kubwa la siku moja au kuanza kuwa na mabishano ama makabiliano.

"Ndoa nyingi au uhusiano huisha kwa maneno mazuri badala ya cheche za moto," anasema McNulty.

Wanandoa wengine "wanaona ni ngumu sana kuzungumzia hili au kushughulikia tofauti zinazozunguka shida kuu wanazokumbana nazo.

Mara nyingi huwafanya kutengana zaidi, na [huwa] kama watu wanaokaa kwenye chumba kimoja kuliko wenzi au wapenzi."

Ndio sababu watu wengine wanaweza kutaka kurudiana na mwenzi wa zamani, au kujaribu kuendelea kushikamana na yule wa sasa.

Kwasababu wakati sisi mara nyingi tunaingia kwenye uhusiano mpya tukitarajia utakuwa bora kuliko uliotangulia, McNulty anahimiza tahadhari: "Ikiwa uko kwenye uhusiano na unafikiria kuondoka, kuwa mwangalifu, kwasababu asilimia 69 ya kinachowazunguka ni tofauti za kudumu na mwenzi mmoja na asilimia 69 ya tofauti za kudumu kwa mwingine."

Kwa hiyo ukirudiana na mpenzi wako wa zamani, angalau wewe tayari utakuwa unajua ni tofauti gani hizo za milele zitakuwepo.

Kurejea kwenye uhusiano wa awali kunaweza kuleta hisia ya kama shida kidogo zimepungua kuliko kukutana na mtu mpya na kuanzia maisha upya.

"Unaendelea pale ulipoishia," anasema Judith Kuriansky, mtaalam wa masuala ya uhusiano na ngono, na profesa msaidizi wa saikolojia na elimu katika Chuo cha Ualimu, Chuo Kikuu cha Columbia, katika Jiji la New York.

Kwa watu wengine, unahisi "vizuri zaidi kurudi kwa mtu ambaye unajua kitu juu yake, kuliko mtu ambaye hajui chochote kumhusu&quot".

Kusherehekea kilichobadilika

Faida nyingine ya kurudiana na mpenzi wako wa zamani ni ufahamu wa kile kilichobadilishwa kwa wakati ambao mmekuwa mbalimbali.

Unaweza kuwa usiyefaidika wakati unachumbiana na mtu mpya kabisa, kwasababu haujui ni vipi wamekua na kubadilika kwa njia nzuri kadiri muda unavyokwenda.

Ukiwa na mtu wa zamani, unapata zaidi ya picha ya zamani na sasa yaani pande mbili.

Kuriansky anasema moja ya sababu kuu za kawaida za wapenzi wa zamani kuhuisha upya mapenzi yao ni "kujisikia kama wamekua na kukomaa"

Violette de Ayala ni Mkurugenzi Mtendaji wa Miami wa shirika la mitandao ya wanawake linaloitwa FemCity, ambaye anazungumziwa hadharani juu ya jinsi alivyoolewa tena na mume wake wa zamani wa miaka 20 mnamo 2019.

"Tulipoanza kuchumbiana tena, ilikuwa nzuri kwasababu tulikuwa tunajuana, lakini mambo kadhaa kati yetu yalikuwa yamebadilika," anasema.

"Sisi wote tulifanyia kazi kwenye maeneo ambayo tulihitaji kufanyia kazi tukiwa tumetengana, na kwa njia nyingi tulikuwa 'wapya' kwa kila mmoja wetu."

"Vipengele vya sisi wenyewe ambavyo vilibadilika viliunganisha tena mchakato mzuri wakati wa kufanyia kazi maumivu kadhaa yaliyotokana na kuvunjika kwa ndoa," anaongeza de Ayala. "Hakujichukulia tena uhusiano wetu kiurahisi tu. Alianza kunipatia zawadi nzuri, na sasa ameanza kushirikisha upendo wake na kuukubali. Hilo haikuwepo mara ya kwanza."

Kinyume chake, ikiwa mmetangana kwa muda mrefu, kurudiana pamoja na ujione kuwa unaangukia katika mifumo ile ile ya awali iliyokuwa sumu kwenye uhusiano wenu wa awali, maarifa hayo yanaweza kuwa ya faida pia.

Kuhisi kuwa utakabiliwa na maumivu yale yale tena, kunaweza kukupa mtazamo wa mapema ili kuepuka maafa sawa na yaliyotokea awali.

'Upendo na mapenzi ya apokalipsi'

Kabla ya kuanza kurejesha uhusiano wa zamani, jiulize kwanini umeamua kufanya hivyo - kwasababu mengi yanaweza kwenda mrama.

Wakati moja ya furaha ya kurudiana na mpenzi wa zamani ni raha au kujuana tayari, Kuriansky anasema kuwa kutamani faraja kunaweza kuchukuliwa visivyo, haswa hivi karibuni kwani tunaonekana kuishi katikati ya malumbano ya kila wakati.

Mnamo mwezi Mei, wakati hatua za kutotoka nje zilikuwa zinaendelezwa, utafiti kutoka Taasisi ya Kinsey ya Chuo Kikuu cha Indiana, ambayo inahusu ngono na uhusiano, ilisea kwamba watu karibu watano walikuwa wakiwatumia ujumbe waliokuwa wapezi wao kipindi wamejitenga peke yao na wanapitia upweke.

"Ninauiita 'upendo na mapenzi ya apokalipsi," anasema. "Ambayo ni, 'hakuna kesho, kwa hivyo, bora nitulie'." Kuriansky amesomea mapenzi wakati wa majanga na ugaidi, na anasema ni kawaida kwa watu kuungana tena na wapenzi wa zamani kwasababu ya "hisia ya kwamba kunaweza kusiwe na kesho - sasa angalia kinachoendelea Afghanistan, majanga ya asili kila mahali, [watu wanahisi kama] kuishi katika hali ya Har-Magedoni ", kwa hivyo wanataka kurudi kwa mtu ambaye wakati mmoja aliwapa upendo na usalama.

Kuriansky pia anashauri kutafuta maoni ya marafiki na familia kabla ya kumfuata mpenzi au mwenza wa zamani. Wengi wanaweza kuwa na mtazamo hasi, haswa ikiwa uhusiano uliisha vibaya. Lakini kusudi la zoezi hili sio kukaribisha hukumu kutoka kwa wapendwa wao; badala, yake wanaweza kukurejesha tena katika madhila uliopitia na kukukumbusha kwanini uhusiano huo ulikuwa na matatizo.

"Kuwa tayari kwa maoni ya watu wengine. Watu wengi watasema, Nini! Mnarudiana? Unatania sio? Kwa nini? Watarejesha tena kumbukumbu zote hizo, kwa hiyo, jiulize, utashughulikia vipi hilo? " anasema Kuriansky.

Wengi wetu tunaweza kujikuta tukitamani upendo uliopotea. Ikiwa tutafanya hivyo kwa njia ya uhalisia, kwa njia yenye kuleta tija, kuna uwezekano mkubwa, tukafanikiwa - ikiwa wahusika wote wana maono na mtazamo sawa.