Jinsi masai wanavyoweza kuishi pamoja na simba

Muhtasari
  • Katika jamii ya kimasai kuua Simba ni jambo linalokufanya upate heshima
  • Kwa muda mrefu Meiteranga Kamumu Saitoti amekuwa na ndoto za kuja kuua simba
Image: BBC

Katika jamii ya kimasai kuua Simba ni jambo linalokufanya upate heshima.

Lakini sasa toka mamlaka zinazoangalia hifadhi nchini Kenya wameweza kurudisha amani kati ya Wamasai na Simba.

Kwa muda mrefu Meiteranga Kamumu Saitoti amekuwa na ndoto za kuja kuua simba.

Akiwa bado kijana mdogo wa aliyeishi kusini mwa Kenya, eneo lenye simba wengi, Kando ya hifadhi ya Amboseli maarufu kwa kuwa na tembo pamoja na simba wengi na taswira ya mlima Kilimanjaro kwa mbali.

Simba na wanyama wengine hupendelea kuzunguka sehemu anayoishi Saitoti.

Jamii ya kimasai ambayo hupendelea kuishi katika eneo moja, pia na tabia yao ya kuhama hama kutafuta malisho ya mifugo yao.

Wakiwa katika hifadhi ya wanyama ya Amboseli, wanyama kama Tembo, swala, fisi na Simba sio nadra sana kuwaona.

Haya bado ni mambo yanaeyoendelea amabapo wanyama wakali kama Simba na chui wanaishi karibu na binadamu na sio wakiwa kwenye uzio wa kuwatenganisha kwa usalama wao.

Masai na Simba wamekuwa wakiishi pamoja kwa karne sasa, jamii ya kimaasai imeendelea kujichukulia kuwa bado wapo thabiti katika kuwakabili Simba hata wanapokutana nao ujasiri ni wosia wanaotembea nao kila uchao.

Katika mila za kimaasai ijulikanayo kama olamaiyo ili mtu atambuliwe kama amepevuka hasa kijana wa kiume ni lazima amuue simba.

Kipindi ambacho Saitoti akiwa bado kijana mdogo, watu wa familia yake walimuadithia mikasa mbalimbali hasa ya kuwa jasiri huku wakimwambia kuwa ili aweze kuwa kijana shupavu kama kaka zake na baba yake ni lazima aue simba, Baba pamoja na wajomba zake wameshawahi kuua Simba 15 enzi za ujana wao.

Saitoti alifanikiwa kuua simba wake wa kwanza akiwa na miaka 19 tu,alijificha katika majani marefu na baadae alifanikiwa kumchoma mkuki, lakini watoto wa simba walifanikiwa kumponyoka.

Pengine sio jambo rahisi kufanyika, lakini ndani ya jamii ya kimasai uwindaji wa simba ni moja ya majukumu ya kuheshimika zaidi.

Hakuna nishani yoyote mtu hupatiwa ikilinganishwa na michezo mengine ambayo timu inapatiwa kombe pale inapokuwa imeshinda bali ushindi mkubwa katika uwindaji wa simba ni ujasiri unaoneshwa na mtu mwenyewe na njia alizotumia kama kuchoma mkuki.

Utamaduni huu umeonakana kuwa hauna maana kwani unachangia sana kupunguza namba ya wanyama hao katika hifadhi.

Kadri miaka inavyozidi kusonga Saitoti amefanikiwa kuua simba wanne.

Amekuwa akitambulika kama mmoja wa muuaji mashuhuri wa simba, pengine uchukuliwa kama shujaa.

Image: BBC

Ndani ya jamii ya kiimaasai hawaamini kama Dunia inaweza ikaishiwa na simba kama wataalamu wanavyosema.

"Kama kusengkuwa na simba huko Maasailand, jambo hili lingekuwa hatari zaidi," alisema Saitoti. "Kishindo cha simba na ngurumo ni ishara ya furaha porini na bahati."

Idadi ya watu katika bonde la Amboseli imekuwa ikiongezeka kila uchao na mwaka 2006 idadi ya simba ilifikia 100 ambao waliishi na wamaasai 35,000 na mifugo milioni mbili.

Simba walianza kuua mifugo zaidi tofauti na vipindi vingine vyote vya mwaka kuanzia hapo wamaasai wakaanza kuua simba na sio kwa kipengele cha mila bali kulinda mifugo yao.

Mwaka 2006 maasai waliwachoma mikuki na kuwapa sumu simba 42, Jambo lilifanya simba wengi kuikimbia Amboseli.

"Kulikuwa na simba wengi sana wakati nikiwa mtoto,"Saitoti anasema, mwaka mmoja baadae "Tuliwamaliza wote."

Kipindi hiko, Saitoti hakuwa na uelewa wa kwanini jamii yake wanaua simba.

Baada ya kuua simba wake wa nne mwaka 2006,Saitoti alikamatwa na kufungwa huku akipigwa faini ya kulipa 70,000 fedha za kenya (sawa na £465);

Ingawa sheria ya uwindaji haramu wa kuua simba imekuwa ikitambulika tangu mwaka 1977.

Muda mfupi baada ya Saitoti kuachiliwa kutoka gerezani, ng'ombe wake wengine walipotea.

Akijua kwamba simba alikuwa amewachukua, akaanza safari, akiwafuata simba wawili kupitia msituni. Saa kadhaa baadaye, aliingia porini kuwasaka na kukuta simba dume wawili wakiwa wamelala alichofanya ni kuwachoma mikuki kifuani.

Huku akigundua kuwa amefanya makosa ya kuua Simba wasiokuwa na hatia waliaambia wadogo zake kuwa hakuna yoyote anayeruhusiwa kushangilia na kweli mikia ya simba hao iliachwa na kurudi nyumbani kama hakuja tokea kitu.

Miezi kadhaa Saitoti alikuwa katika kipindi kigumu sana. Hakumwambia mtu yoyote yaliokuwa yanamsibu.

Alikataa kujumuika na wenzake katika uwindaji jambo lililowatia wasiwasi.

Walianza kumuita majina ya kumdogosha kama vile muoga' alikasirishwa na fedheha alizokuwa anazipata lakini aliendelea kuwa mvumilivu huku akitambua kuwa wale ni simba wake wa mwisho kuwaua.

Ulikuwa ndio muda ambao Saitoti alianza kusikia mpango wa uhifadhi ambao ulikuwa umeanza kufanya kazi katika eneo hilo.

Ukiitwa Walinzi wa Simba Lion Guardians,, vijana mashujaa wa Kimasai ambao waliwahi kuua simba ndio walianza kutumika kama wakawa walinzi wa simba ndani ya jamii za Wamasai.

Kama moja ya mipango, wamaasai walifanya kazi na watunzaji wa mazingra wakimarekani Dr Leela Hazzah na Dr Stephanie Dolrenry.

Mwaka mmoja baadae Dolrenry aikutana na Saitoti, alivyomuona alipiga makelele kuwa "ndio huyu tunamtaka anaonekana kama ameshaua Simba."

Wote walifahamu kuwa ili mpango wao wa kulinda wanyama uweze kufanikiwa ni muhimu kuwapata wale ambao walihusika moja kwa moja kuua simba na kuitwa mashujaa katika jamii zao, Saitoti akachaguliwa kuwa miongoni mwa waliotakiwa na moja kwa moja akaanza kazi yake ya kulinda simba.

Wapiganaji kama Saitoti walikuwa wameonyesha utaalam wao katika kufuatilia simba ili waweze kuwaua. Lakini katika majukumu ya malezi ya Simba walifuatilia ng'ombe waliopotea na kuwaonya wengine waepuke kufika maeneo ambayo simba walikuwepo.

Vijana waliokuwa mashujaa wa kuua Simba sasa wakaanza kuwa mashujaa wa kuwaambia wafugaji katika jamii zao kuepuka maeneo yaliokuwa yanatembelewa zaidi na simba. walifanya hivyo kwa lengo la kusaidia kuweka mifugo na wafugaji wao mbali na simba.

Na ambapo vijana wa Kimasai hapo awali walionyesha ujasiri wao kwa kuua simba, sasa walifanya hivyo kwa kuwazuia Wamaasai wenzao wasiende kwenye uwindaji wa simba.

"Kuzuia uwindaji wa simba ni ngumu zaidi kuliko kumkabili simba mwenyewe," Saitoti alisema, licha ya kuwa na uzoefu wa kufanya vyote kwa pamoja.

Katika safari yake ya kwanza kama Mlinzi wa Simba katika Hifadhi ya Selenkay, Eneo lenye kundi kubwa la Wamaasai kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa ya Amboseli, Saitoti alianza kumfuatilia simba mmoja.

Mwanzoni, hakuna mtu aliyeelewa ni kwanini simba, usiku mmoja yeye na Dolrenry walimchukua simba, wakamweka iliyowawezesha kupata taarifa zake kisha wakamwacha huru.

"Katika tamaduni zetu, unapofanikiwa kuua simiba wako wa kwanza, utapewa jina la simba huyo na kuishi nalo milele," Hazzah akielezea.

Saitoti alipewa jina la Meiteranga linalomaanisha "Huyu ndie wa kwanza" baada ya kuua simba wake wa kwanza."Sasa anahusika katika kuwasaka Simba na kujimilikisha. Wanawapatia majina."

Saitoti alipatia kitoto cha simba jina la Nosieki. Simba huyu alikuwa mtoto wa mmoja wa wale ambao Saitoti aliuua akiwa na miaka 19, lakini sasa ameapa kumhudumia mtoto huyo wa simba.

"Baada ya kuua simba nikitimiza wajibu wangu wakiutamaduni,kuonesha watu mimi ni shujaa," Alijibu Saitoti baada tu ya kubadilika na kuwa mlinzi wa Simba. " Jambo hili linaniheshimisha zaidi kuliko awali , kwasasa nawalinda kama vile nilivyokuwa nawawinda kuwaua."

Mpango wa kulinda Simba, Saitoti akiwa ni miongoni.

Ulianzishwa mwaka 2007 ukiwa na waangalizi watano tu.

Hasa kwenye maeneo ambayo yanashughuli za kibinadamu na hifadhi. Mpango huu umeonekana kuwa ni wenye mafanikio, mwaka 2018 hakuna Simba hata mmoja aliyeuwawa kwenye eneo analolindwa.

Idadi ya Simba imeanza kuleta nuru baada ya kuongezeka mara sita zaidi tokea mpango kulinda simba uanze, kwasasa waangalizi hao wanafanya kazi katika eneo lenye ukubwa wa 4,0000 km.

Miongo kadhaa sasa imepita , Saitoti yupo mbioni kustaafu ameonesha nia yake ya dhati katika kuwafundisha vijana wa njia za kisasa za ufugaji bila kusahau tamaduni za kimaasai huku akija kivingine zaidi kwa kuhubiri njia za kuwalinda viumbe hai wengine walio karibu na makazi yao.

Licha ya kuwa mmoja wa wauaji wakubwa wa Simba, yeye pamoja na wenzake chini ya mpango wa kuwalinda simba wanaacha alama isiyofutika ya kuwaokoa simba pamoja na mifugo katika jamii ya kimaasai.