Fahamu madini ya thamani yaliojaa kwa simu yako ya zamani usioitumia

Image: GETTY IMAGES

Kuna dhahabu, platinamu na vifaa vingine vya thamani katika kila simu - kigumu ni kutoa sehemu hizo.

Simu aina ya iPhone yenye almasi inaweza kukurejeshea $ 95m - lakini ikiwa kipande hiki cha johari hakina bei uliko, usijisikie kukata tamaa.

Kila simu aina ya smartphone ina madini ya thamani ikiwa ni pamoja na dhahabu, fedha, shaba, platinamu na paladi.

Hii ni zaidi ya maelezo ya kufuraisha juu ya kifaa ambacho huwa nawe kila wakati.

Vito hivi vya thamani sasa vinaonekana kuwa vya thamani zaidi kuliko hapo awali, kwani tunakabiliwa na matarajio ya siku moja tutakosa uwezo wa kuzichimba kutoka ardhini.

Ghafla smartphone yako inaonekana yenye thamani zaidi kuliko unavyofikiria.

Thamani iliyofichwa ya vito vya ndani vya vifaa vyetu vya zamani vya kielektroniki, na jinsi tunavyoweza kupata vifaa hivyo vya ndani ni moja wapo ya mada ambayo itajadiliwa katika mkutano wa BBC unaoangazia mawazo yanayobadilika duniani utakaofanyika huko Sydney mnamo mwezi Novemba.

Nini hasa kilichopo ndani ya Smartphone yangu?

Simu za smartphone ni vito vya mfukoni na adimu duniani.

iPhone ya kawaida inakadiriwa kuwa na karibu 0.034g ya dhahabu, 0.34g ya fedha, 0.015g ya paladi na chini ya gramu moja ya gramu ya platinamu.

Pia ina alumini isiyo na thamani lakini bado muhimu (25g) na shaba (karibu 15g).

Kuanzia simu za mkononi hadi kompyuta, Guiyu nchini China ndio mji unaopokea taka nyingi za kielektroniki ulimwenguni - mnamo mwaka 2008, hadi 80% ya nyenzo zilichakatwa huko kutoka mataifa mengine duniani
Kuanzia simu za mkononi hadi kompyuta, Guiyu nchini China ndio mji unaopokea taka nyingi za kielektroniki ulimwenguni - mnamo mwaka 2008, hadi 80% ya nyenzo zilichakatwa huko kutoka mataifa mengine duniani
Image: GETTY IMAGES

Na huo ni mwanzo tu.

Simu za mkononi pia zina madini kadhaa nadra sana ulimwengu - vitu ambavyo ni vingi kwenye ganda la Dunia lakini ni vigumu sana kuvichimba na kupata faida yake kiuchumi - ikiwa ni pamoja na yttriamu, lanthanamu, terbiamu, neodymiamu, gadolinium na praseodymiamu.

Halafu pia kuna plastiki, glasi, betriā€¦ ni orodha ndefu sana ya vitu.

Hizi zote zipo kwa kiasi kidogo. Lakini zaidi ya watu bilioni mbili hivi sasa wana smartphone, na idadi hiyo inakadiriwa kuongezeka.

Isitoshe, mkusanyiko wa baadhi ya vitu hivi, kama dhahabu na fedha kwenye simu ya rununu ni wa kiwango cha juu sana kuliko

Tani moja ya iphone ingeweza kutoa dhahabu mara 300 zaidi ya tani ya madini ya dhahabu na fedha mara 6.5 zaidi ya tani ya madini ya fedha.

Kwanini hili ni tatizo?

Kwasababu wale watumiaji bilioni mbili wa simu za smartphones wanabadilisha na kuanza kutumia simu mpya ya kisasa zaidi iliyoboreshwa takribani kila miezi 11, ambayo inamaanisha smartphone ya zamani hutupwa kwenye droo au mahali pengine na kusahaulika, au hutupwa nje.

Ni asilimia chache sana yaani kama 10 ya simu hizi huchakatwa tena na vitu vyao vya thamani vinapona na kutumiwa tena. Na ijue kwamba ni madini ya dhahabu ya kweli yaliyokaa kwenye kabati, kwenye masanduku, kwenye takataka.

Nini kinatokea kwa rasilimali hizi wakati simu inakuwa haifanyi tena kazi?

Ikiwa unafikiria kujaribu uchimbaji wa dhahabu kidogo kwa kiwango cha mtu binafsi, kiasi kidogo katika kila smartphone inapaswa kukufanya ufikirie mara mbili.

Lakini mara tu unapoanza kufikiria kwa kiwango kikubwa, inaonekana kuvutia zaidi: simu milioni moja za mkononi zinaweza kutoa karibu tani 16 za shaba, 350kg ya fedha, 34kg ya dhahabu na 15kg ya paladi.

Changamoto ni jinsi ya kurejesha madini na vifaa hivyo salama na kiuchumi.

Sehemu kubwa ya takataka za kielektroniki - ikiwa ni pamoja na simu za rununu - huuzwa au kutupwa katika nchi kama Uchina ambapo wafanyikazi na watoto wanaolipwa pesa kidogo wanaripotiwa kutumiwa kuvunja vifaa hivyo vya elektroniki na mara nyingi wakitumia kemikali hatari kupata vitu muhimu.

Mji mmoja kusini mashariki mwa China uitwao Guiyu umedai kutiliwa shaka ya kuwa kitovu kikubwa cha taka za kielektroniki ulimwenguni.

Hilo linasababisha matatizo mabaya ya kiafya kwa wakaazi wake na uchafuzi wa mazingira, mito na hewa kwa zebaki, madini yenye sumu kama aseniki, kromiamu na yale ya risasi.

Hata takata za kielektroniki ambazo zinachakatwa tena katika nchi yake ya asili kuna changamoto.

Kwa mfano, huko Australia, kuchakata tena taka za kielektroniki bado kunahusisha kuyeyusha vyuma viwanda ambako ni gharama kubwa na pia kunachafua mazingira.

Vifaa vya kielektroniki vina vito vingi vya thamani ambavyo ni adimu kupatikana, lakini vingi hutolewa katika hali ya uchafuzi wa mazingira na maeneo yenye sumu kama vile Guiyu nchini China.
Vifaa vya kielektroniki vina vito vingi vya thamani ambavyo ni adimu kupatikana, lakini vingi hutolewa katika hali ya uchafuzi wa mazingira na maeneo yenye sumu kama vile Guiyu nchini China.
Image: GETTY IMAGES

Je kuna njia bora ya kukabiliana na hili?

Bila shaka, kua njia nyingine. Kwanza, tunaweza kuacha kubadilisha simu za mkononi ndani ya kipindi kifupi kuliko tunavyobadilisha nguo zetu za ndani.

Lakini kwa kutambua kuwa kubadilisha tabia ya watumiaji labda ni miongoni mwa machaguo ya chini zaidi tunayoweza kuchukua, tunahitaji kupata chaguo bora zaidi.

Mwanasayansi wa vifaa vya elektroniki Veena Sahajwalla kutoka Chuo Kikuu cha New South Wales anachukua njia ndogo kutatua tatizo la kiulimwengu.

Njia yake haiitaji mwingilio wa moja kwa moja, kupunguza hitaji la mawasiliano ya kibinadamu na vifaa hatari zaidi ndani ya simu ya mkononi.

Simu yake ya mkononi imevunjwa kwa kutumia nguvu ya juu ya umeme.

Halafu vile vitu vya thamani hutolewa kwa mkono wa roboti, na kuwekwa ndani ya tanuru ndogo ambayo kiwango chake cha joto kinadhibitiwa kwa usahihi kutoa vito vya thamani ndani yake.

Vifaa vyovyote vyenye sumu au visivyohitajika vinachomwa kwa njia salama.

Nani anayejua - fanya hivyo kwa kipidi kirefu na unaweza kujijengea mazingira ya kuwa na dhahabu yako ngumu, smartphone iliyotiwa almasi.