Kwa nini dhana ya "kupoteza ubikira" inapaswa kupuuzwa?

Muhtasari

•Wataalamu wa elimu wanaamini kwamba dhana hiyo haiwakilishi uzoezu wa watu wengi sasa.

Image: GETTY IMAGES

Dhana kuhusu "ubikira" imekua tata.

Watetezi wa wanawake wanasema dhana ya kutunza ubikira kwa kawaida ilikuwa kama hazina, zawadi, au ukumbusho ambao wanawake "hutoa," "kuchukua," au "kupoteza"

Wataalamu wa elimu wanaamini kwamba dhana hiyo haiwakilishi uzoezu wa watu wengi sasa.

Ingawa wengi wanaamini kwamba dhana hii ina matatizo, wachache wamekuja na na dhana mbadala.

Mwaka jana, Nicolle Hodges , anayejitambulisha kama "mwanafalsafa wa uhuru wa kijinsia" kutoka Toronto, Canada, alileta dhana mpya kupinga dhana iliyokuwepo ya ubikira, akisema dhana hiyo ni muhimu.

Safari ya dhana yake

Dhana yake ilianza na Dr. Seuss (mwandishi Mmarekani na mchora vibonzo).

Mwaka 2020, Hodges alichapisha "Oh the Places You'll Go Oh, Oh!", kitabu kuhusu nguvu ya kufika kileleni au mshindo wa mwanamke.

Image: GETTY IMAGES

Kwa kutumia kitendo cha kufanya mapenzi kama safari ya kuelekea kwenye dhana yake, Hodges akagundua kwamba anahitaji mahala pa kuanzia.

"Bado tuna hili neno la zamani lenye nguvu," anasema Hodges. "Inakinzana sana dhana na mawazo mapya."

Badala yake, tuondoe ubikira tuweke: "kujamiiana kwa mara ya kwanza."

Hii sio mara ya kwanza neno hili kutumia, lakini Hodges anabaini kwamba inafaa katika mchakato wake wa kubadilisha dhana hiyo.

Ana matumaini kwamba hakuna mabadiliko makubwa zaidi ya neno lenyewe, anasema alishangazwa alipoona wasomaji wakimtaka aitanue zaidi dhana yake hiyo mpya.

Kwa maana hiyo, Hodges akawatumia wafuasi wake kwenye mtandao wa kijamii kama washawishi chanya wa masuala ya mapenzi kuanzisha kampeni yake kuanzisha dhana ya 'kujamiiana kwa mara ya kwanza' kama mbadala wa dhana ya ubikira.

Baada ya mfululizo wa machapisho yake kwenye Instagram na Twitter kuhusu suala hilo, akazindua fulana zake zenye ujumbe wa kampeni hiyo ya kufanya mabadiliko ya dhana.

Awamu inayokuja ya kampeni itahusisha utoaji wa matangazo mbalimbali kuitangaza dhana ama wazo lake hilo pamoja na mfululizo wa video za mahojiano zinazoonesha namna watu walivyopokea wazo hilo la kuwa na dhana ya 'Kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza' badala ya ubikira.

Uzoefu wa ushirikishaji na kuwezesha

Mitandao ya kijamii imebeba kampeni hiyo ya Hodges ya kubadili dhana ya ubikira ikiibua mijadala mbalimbali kuhusu uzoefu wa kujamiiana kwa mara ya kwanza.

Ingawa dhana hiyo imekutana na ukosoaji, majibu ya ujumla yamekuwa kama ya shukrani.

Nicolle Hodges anaendesha kampeni ya kubadilisha dhana ya ubikra na kuitwa 'kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza'
Nicolle Hodges anaendesha kampeni ya kubadilisha dhana ya ubikra na kuitwa 'kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza'
Image: Nicolle Hodges

Kwa wengi wanaounga mkono wazo ama kazi hiyo ya Hodges, ubikira kama dhana ilikuwa ni jambo muhimu kwao na uzoefu wao.

Dhana hii ya Hodges, ya 'kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza' inatoa ufafanuzi rahisi wa moja kwa moja kuhusu uzoefu wa kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza, kitu kimoja ambacho Hodges ana matumaini nacho ni kuhusu ushirikishwaji na kuwezesha.

"Kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza' ulioonyeshwa katika machapisho mengi ya wasomi katika miaka ya 1970 na 1980
"Kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza' ulioonyeshwa katika machapisho mengi ya wasomi katika miaka ya 1970 na 1980
Image: GETTY IMAGES

Kampeni ya Hodges' campaign, inalenga kuondoa dhana ya aibu kwa kulitamka neno 'bikra' na kuleta neno kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza na kutumia neno hili jimpya "hailazimishi kusema ubikra kwamba ndio mwisho wa safari."

"Hii haimaanishi kubadili tu neno 'ubikra' na kuleta neno jipya, lakini anasema ubikra ni dhana ambayo haipo kwa sababu safari yako ya kufanya mapenzi haina mwisho."

"naweza kuwa wakati ule kama wewe binti ama mwanamke, unambusu mwenzio, na mwili wako kuhisi tofauti," anasema.

"Huko ndiko kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza: unashuhudia mabadiliko uelewa wako na mabadiliko yao binafsi.

Je ni jambo rahisi?

Wakati kampeni ya Hodges ilipoanza kwenye mitandao ya kijamii, Julia Feldman-DeCoudreaux alikuwa na mashaka.

Haishawishi vya kutosha kusema ubikira ni dhana iliyopitwa na wakati.

"Ukiangalia jina mbadala la ubikira, bado tunahitaji mjadala mpana kuhusu dhana hiyo ," anasema Feldman-DeCoudreaux.

"Unapotumia neno kama bikira,au kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza, unakuwa unazungumzia kuhusu jambo linaloweza kumgusa mtu mwingine," anafafanua Feldman- DeCoudreaux.

"Tuna jukumu la kufikiria upya kuhusu masuala haya, kwa sababu italeta uzoefu mzuri kwetu sote kama tutaachana na dhana hizi mbaya," anasema Feldman-DeCoudreaux.