'Perfect man': Je mwanaume mwenye muonekano wa kuvutia na aliyekamilika anafananaje?

Muhtasari
  • Je mwanaume mwenye muonekano wa kuvutia na aliyekamilika anafananaje?
Image: BBC

Nini kinachofanya mwanaume anonekane mwenye kuvutia au mzuri? Katika miongo iliyopita, vitu maarufu vya urembo wa mwanaume wa Magharibu ulishabihiana na watu wenye muonekano wa watu maarufu kama Brad Pitt au Leonardo DiCaprio. Lakini suala la 'mwanaume sahihi" aliyekamilika anavyoonekana ni kama sinema na ulimwengu wa mitindo unakubaliana na kuelewa kuhusu utofauti mkubwa uliopo na umuhimu wa uwakilishi wake.

Ulimwenguni kote, muonekano wa sura ya kiume hainakisi mwili wa mwanaume au wanaume wenye miili ya wastani. Lakini kuwepo kwa mitandao ya kijamii kama TikTok kumesaidia kubadili viwango vya urembo wa mwanaume kwa kuwaonyesha wanaume ambao huko nyuma wasingepata fursa hiyo ama jukwaa la kuonekana.

Mwanamitindo Muingereza na mwanaharakati maarufu wenye mtandao wa TikTok Ben James anabadili namna wanaume wenye miili mikubwa walivyokuwa wanachukuliwa. Mwaka 2019, akiwa mwanamitindo mwenye mwili mkubwa, alishiriki katika tangazo moja linalotangaza mavazi ya chapa ya Simply Be, akionekana pamoja na wanamitindo wengine mbalimbali, alifanya kazi pia na Ted Baker na Asos. James ameiambia BBC Culture kwamba kazi yake "inawapa vijana na wanaume wenye muonekano mkubwa kama wake faraja na kujiamini na kwamba wana tahamani pia ".

Hatuwezi kuwa na watu wenye maumbo ya kibaba 'vitambi' kwenye kampeni ama matangazo ya manukato?

Wakati wanawake maarufu wenye maumbo makubwa kama Lizzo na mwanamitindo Ashley Graham wamekuwa maarufu na kufurahiwa kila mahali, wenzao wa kiume wenye maumbo kama yao, wamekuwa gizani. Ingawa hivi karibuni kupitia kazi yake ya Savage Fenty, mwanamuziki Rihanna kama amepooza hali hiyo kwa kuwapa nafasi wanaume wenye maumbo makubwa na wanene.

Je hiyo ni ishara ya kukua kwa sekta ya urembo wa mwanaume?

Kwa maana nyingine ni ishara ya kuongezeka kwa urembo wa mwanaume? Ben James analieleza hilo: "Ningetamani kuona sekta hii inaboreshwa kwa kuwepo kwa watu wenye maumbo tofauti tofauti ambao hayajawahi kuonekana huko nyuma. Kwa nini hatuwezi kuwa na watu wenye maumbo ya kibaba 'vitambi' kwenye kampeni ama matangazo ya manukato? Au kuongoza kwenye filamu?

Mtazamo ama muelekeo unabidi ubadilike kutoka kwa wanaume wenye misuli ambayo hawawezi kudumu nayo".

Profesa kutoka chuo kikuu cha Edinburgh, Alexander Edmonds, ameiambia BBC kwamba: "Kwa sababu ya utumwa na ukoloni wa watu wa Magharibi, muonekano wa mwanaume mzuri siku zote umekuwa ni ule mweupe, na huko nyuma kulikuwa na vizingiti vichache kwa hili kubadilika, lakini sasa linawezekana".

Wanamitindo maarufu weusi kama Tyson Beckford na Alton Mason mara nyingi wameuonekana kwenye ukurasa wa mbele wa majarida kama GQ na mengineyo ya masuala ya urembo, kwa kiasi Fulani kidokidogo inaonekana utofauti zaidi, pengine kiasi kwa sababu mabadiliko na misukumo ya kijamii kwa mfano kampeni ya 'Black Lives Matter' zimeifanya chapa hiyo kutambua umuhimu wa utofauti wa watu.

"Muonekano wa uzuri na tabia ya mwanaume unabadilika," anasema Edmonds. "Hauko tena kwa vijana. Hii inatokea Mashariki mwa Asia hasa kwenye jamii ya wanamuziki wa Pop wa Korea Kusini". Nchini Korea Kusini, linaonekana kama suala la kike, kwa makundi ya muziki ya K-Pop kama BTS, wanaotambulika kwa namna wanavyotengeneza nywele zao na kujiremba. Urembo wa aina hii unachukuliwa kama ni utamaduni wa magharibi - lakini sas

Urefu, weusi na uzuri kwa wanamitindo maarufu

Wanamitindo maarufu wa kiume wanaonekana kwenda sawa na wenzao wa kike kimafanikio na wanaonekana kupata nguvu na ushawishi katika miaka ya hivi karibuni.

Mwanamitindo wa Marekani Tyson Beckford alipata mkataba wa Ralph Lauren kutangaza brandi hiyo na toka wakati huo amekuwa mwanamitindo mweusi maarufu zaidi wa muda wote. Mwanamitindo mwingine Sean O'Pry, kwa upande wake, aliyedumu kwenye uanamitindo kwa miaka zaidi 15, na kumfanya kuwa mwanamitindo wa kiume tajiri zaidi duniani.

Akitokea kwenye Georgia, Marekani aliwasili New York akiwa na umri wa miaka 17 na akiwa na dola $150 mfukoni kwake - akapata mikataba minono kutoka kwenye makampuni makubwa.

O'Pry alipata umaarufu kupitia video ya mwanamuziki Taylor Swift ya mwaka 2014 iliyoitwa Blank Space."Ni jambo kubwa kwenye maisha yangu," O'Pry ameiambia BBC. "Sikujaribu kujibadilisha muoekano wangu."

Kuna nadharia ya muonekano wa watu wa Mediterrana "Urefu, weusi na uzuri" unahitajika sana, licha ya kuongezeka kwa utofauti wa muonekano wa watu. Mtaalam Shafee Hassan anaiambia BBC kwamba: "Wanaume wa Mediterrania wana faida kubwa kwa kuwa na nyusi za kahawia na nywele nyeusi.

Unaweza kufuga ndevu… nywele nyeusi zinazohusiano na uanaume".

Mfano mzuri wa hivi ni muigizaji kutoka Italia Michele Morrone. Akitokea Puglia, Kusini mwa Italia alikuwa akifanya kazi kama muhudumu wa bustani huko Roma mpaka mwaka jana aliposhiriki mashindano ya kumsaka muigizaji. Maisha yake yakabadilika ghafla baada ya kufanikiwa kupata nafasi ya kucheza filamu ya Netflix ya 365 Days.

Licha ya mafanikio kuendelea ya urembo wa mwanaume uliozoeleka, Urembo wa mwanaume wa kawaida sasa unakuwa na kufunguka. Wanamitindo wenye umri mkubwa wanaonekana kupata umaaarufu mkubwa.

Tulizoea kuwaona wanamitindo kama Pierce Brosnan na George Clooney lakini sasa wanamitindo wenye umri mkubwa wamekuwa akitumika kwenye matangazo mengi miongoni mwao ni Anthony Varrecchia, Wang Deshun (ambaye anajulikana kaa "Babu mwenye mvuto zaidi China"), Ron Jack Foley na Lono Brazil.

Mwaamitindo mwenye umri wa miaka 87 René Glémarec alionekana akiwa na mkewe mwenye miaka 86 Marie-Louise, kwenye wiki ya mavazi huko Parisris wakiwa na mavazi yaliyotengenezwa na mjukuu wao Florentin Glémarec.

Mwanamitindo Orlando Hobechi hivi karibuni aliiambia the Guardian: "Miaka minne iliyopita niligundua kuongezekakwa matumizi ya wanamitindo wenye umri mkubwa. SGhafla watuwanataka kusikia kuhusu habari za watu wazee. Kwa miaka zaidi ya 30, tumekuwa tukishuhudia vijana - unaweza kuwa mtu mzima na bado ukafaa … watu wanataka kuona watu ambao wanamuonekano kama wao wanawakilishwa."